2021
Imani Itahamisha Milima
Mei/Juni 2021


Ujumbe wa Mkutano kutoka kwa Nabii

Imani Itahamisha Milima

Imetoholewa kutoka “Kristo Amefufuka; Imani Kwake Itahamisha Milima,” Liahona, Mei 2021.

Picha
May 2021 Friend

Kila kitu kizuri maishani—na kila baraka—huanza na imani. Katika Biblia, Yesu aliahidi kwamba “tukiwa na imani kiasi cha punje ya haradali,” tutaweza kuhamisha milima (Mathayo 17:20). Milima yako inaweza kuwa upweke, mashaka, magonjwa, au shida zingine.

Mbegu ya haradali inawakilisha imani ndogo lakini inayokua. Mbegu ya haradali huanza kidogo lakini hukua na kuwa mti mkubwa wa kutosha kwa ndege kujenga viota kwenye matawi yake. Ninawaomba muanze leo kuongeza imani yenu. Hizi ni baadhi ya njia za kujenga imani na tumaini lenu.

  1. Jifunze kuhusu Yesu Kristo kwa kusoma maandiko. Jifunze kuhusu miujiza Yake.

  2. Chagua kuamini katika Yesu Kristo. Fikiria kuhusu Yesu Kristo kila siku.

  3. Tenda kwa Imani. Chagua kubatizwa na shiriki sakramenti.

  4. Muombe Baba wa Mbinguni akusaidie.

Imani yako katika Yesu Kristo itahamisha milima. Imani itakusaidia kuzigeuza changamoto kuwa fursa za kupendeza.

Yesu Kristo Amefufuka

Picha
May 2021 Friend

Chapisha