2021
Yesu Aliwajumuisha Wengine
Mei/Juni 2021


Kusaidia Kama Yesu

Yesu Aliwajumuisha Wengine

Picha
Jesus with children

Siku moja kikundi cha watoto walikuja kumwona Yesu Kristo. Wafuasi Wake waliwaambia waondoke. Lakini Yesu akawaambia, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu” (Marko 10:14). Hakutaka kuwaacha. Alitaka kukaa nao kwa sababu aliwapenda.

Mwokozi aliwabeba wale watoto mikononi Mwake. Aliwabariki. Aliwasaidia kujisikia kuwa wao ni watu muhimu.

Picha
A portrait of Kanyin

Nilijisikia mpweke wakati wa mapumziko, hivyo nilimwomba mtu mmoja kama angeweza kucheza na mimi. Tulianza kucheza kwa kutumia chaki, na watu zaidi wakaongezeka, na ilikuwa ya kuburudisha sana! Kama unajisikia mpweke, unaweza kumwomba mtu fulani kucheza na wewe.

Kanyin P., umri miaka 8, Colorado, Marekani

Picha
May 2021 Friend

Chapisha