2021
Watakatifu Wanajenga Makazi Mapya
Mei/Juni 2021


Hadithi za Maandiko

Watakatifu Wanajenga Makazi Mapya

Picha
early Church members being baptized

Baada ya Kanisa kurejeshwa, watu wengi zaidi na zaidi walijifunza kuhusu injili. Walichagua kubatizwa. Waliitwa “Watakatifu.”

Picha
pioneer children talking together

Baadhi yao walihama ili waweze kuwa karibu na waumini wengine wa Kanisa. Watakatifu walisaidiana na kuimarishana.

Picha
pioneer family leaving home

Watu wengine hawakulipenda Kanisa. Walijaribu kuwaumiza Watakatifu. Waliwalazimisha kuziacha nyumba zao.

Picha
pioneer children carrying wood

Watakatifu walikuwa na imani kwamba Mungu angewasaidia. Ingawa ilikuwa vigumu, walihamia kwenye eneo jipya. Walifanya kazi kwa pamoja ili kujenga mji mpya.

Picha
family visiting grandma in hospital

Ninaweza kuyakabili mambo mapya kwa imani. Ninaweza kuwasaidia wengine pia wakati wa nyakati ngumu.

Chapisha