2021
Nitamwona Kaka Yangu Tena
Mei/Juni 2021


Imeandikwa na Wewe

Nitamwona Kaka Yangu Tena

Picha
girl hugging Primary teacher

Wiki ile nyingine ilikuwa siku ya kuzaliwa kwa kaka yangu mdogo Gabrieli. Angekuwa na miaka saba, lakini alikuwa na ugonjwa wa kupooza na alifariki miaka miwili iliyopita. Katika Msingi tuliimba “Gethsemane.” Maneno yalikuwa wazi na yenye kuleta maana. Yalikijaza chumba kwa Roho.

Baada ya wimbo, Dada Webster alitoa ushuhuda juu ya Upatanisho wa Yesu Kristo. Ulikijaza chumba kwa Roho zaidi. Kisha alizungumzia kuhusu jinsi kaka yake alivyofariki miaka kadhaa iliyopita. Ilinifanya nimfikirie Gabrieli, na karibia nianze kulia. Nilifikiria kuhusu wakati nilipombeba Gabi kwa mara ya mwisho. Nilikuwa mwenye huzuni, lakini pia nilisikia amani.

Dada Webster alizungumzia kuhusu jinsi alivyo na furaha kwa kujua kwamba angemwona kaka yake tena. Alisema alijua sisi sote tungewaona wapendwa wetu waliofariki dunia.

Baada ya Msingi nilimpa Dada Webster kumbatio. Tulilia pamoja kwa dakika chache. Roho alikuwa na nguvu nyingi. Aliniambia kwamba ningemwona kaka yangu mdogo tena. Alisema Upatanisho wa Yesu Kristo siyo tu kwa walio waovu bali pia kwa wanaoumia. Aliniuliza ni kitu gani nakikosa hasa kutoka kwa Gabi, nami nilisema kwamba hakika nlikosa kicheko chake.

Nilimwambia Dada Webster kwamba nimekuwa mwenye huzuni kwa sababu siku ya kuzaliwa kwa Gabrieli ilikuwa wiki hiyo na hakika nilihitaji kujua kwamba ningemwona tena kaka yangu. Aliniambia machozi yale tuliyokuwa tumelia yalikuwa machozi ya furaha. Niliweza kumhisi Roho, na nilijua alichokisema kilikuwa cha kweli. Ninao uhakika kwamba nitamwona Gabrieli tena, na hilo linanifanya niwe na furaha sana. Ninampenda. Ninajua kwamba kwa sababu Yesu Kristo ananipenda, aliutoa uhai Wake ili kwamba niweze kumwona Garieli tena.

Chapisha