Mikono ya Usaidizi kote Ulimwenguni
Kutana na Shilohkutoka Ufilipino
Kutana na watoto wa Msingi wakiwasaidia wengine, kama Yesu alivyofanya.
Yote kuhusu Shiloh
Umri miaka: 7
Kutoka: Ufilipino
Lugha: Kifilipino, Kiingereza
Familia: Mama, Baba, na ndugu wengine watatu wakubwa
Malengo na ndoto: 1) Daima kuwatumikia wengine.2) Kuwa mcheza dansi.3) Kuwa mpishi mwenye mafanikio.
Mikono ya Usaidizi ya Shiloh
Shiloh anapenda kuwasaidia watu popote anapokwenda. Yeye ana urafiki mkubwa na wanafunzi wa darasa lake shuleni. Bila kujali tofauti walizo nazo. Yeye anajua kuwa kila mmoja ni mtoto wa Mungu! Shiloh anayo hali inayoitwa Down syndrome, na rafiki yake wa karibu zaidi, Kharl, hawezi kutembea. Shiloh daima anamsaidia Kharl na kitimwendo chake.
Shiloh daima yuko tayari kucheza na kila mmoja, hata na watoto ambao bado hawajui vizuri. Anapenda kutengeneza marafiki wapya. Wakati mmoja familia yake ilipokwenda kutembelea Hekalu la Manila, Ufilipino, alimwona msichana katika chumba cha kusubiria ambaye hakuwa na mtu wa kucheza naye. Alikwenda na akaanza kucheza naye. Hata alishiriki naye tableti yake.
Mambo Ayapendayo Shiloh
Mahali: Uwanjani
Hadithi kuhusu Yesu: Wakati alipowabariki watoto wadogo.
Wimbo wa Msingi: “Keep the Commandments“ (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 146–47)
Chakula: Chipsi, samaki, mayai, na wali
Rangi: Samawati
Somo shuleni: Hisabati