2021
Hisia ya Amani
Septemba 2021


Rafiki kwa Rafiki

Hisia ya Amani

Kutoka kwenye mahojiano na Lucy Stevenson Ewell.

boy sitting in garden on bench with teacher

Asubuhi moja nilipokuwa na umri wa miaka 11, niliiamka na kusikia sauti sebuleni. Hakuna aliyekuja kuniamsha niende shule kama ilivyokuwa kawaida. Nilipotoka nje ili kuangalia kile kilichokuwa kinaendelea, niligundua kwamba baba alikuwa amefariki.

Wakati familia yangu wakiongea sebuleni, mimi nilienda kwenye bustani yetu. Bustani yetu ilikuwa kubwa, na nilikuwa nikifanya kazi pamoja na baba yangu kuitunza. Nikakaa kwenye benchi chini ya mti na kulia. Nisikia huzuni sana na kuchanganyikiwa.

Baada ya dakika chache, nimwona mwalimu wangu wa Msingi akifungua lango. Alikuja na kukaa kwenye benchi karibu nami na kusema, “Joni, unakumbuka somo tulilokuwa nalo Jumapili iliyopita kuhusu mpango wa wokovu?” Mwalimu wangu alinielezea tena kwamba nafsi zetu zina roho na mwili. Alisema kwamba roho ya baba yangu ilikuwa mahali pazuri, na siku moja atafufuliwa. Siku moja ningemwona tena.

Ingawa nilikuwa bado nina huzuni sana, nilijisikia amani. Ninakumbuka amani hiyo kila mara ninapofikiria kuhusu tukio hilo. Mwalimu wangu wa Msingi alinihudumia, na Roho Mtakatifu alinifariji. Ilisaidia kujenga ushuhuda wangu juu ya upendo wa Baba wa Mbinguni na mpango wa wokovu.

Bila kujali kile unachokabiliana nacho, Mungu anakujali. Hauhitaji kuwa mtu mzima kumsikia Roho akishuhudia kwamba kila kitu kitakuwa SAWA. Unaweza kujenga ushuhuda wa mpango wa Baba wa Mbinguni. Unaweza kuhisi amani.

Friend Magazine, 2021/09-10 Sep/Oct Tier 2

Vielelezo na Arthur Lin