2021
Yesu Kristo Alilipatia Jina Kanisa Lake
Septemba 2021


Hadithi za Maandiko

Yesu Kristo Alilipatia Jina Kanisa Lake

Picha
image of Jesus

Bwana alimwambia Joseph kile cha kuliita Kanisa. Alisema lingeitwa “Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.”

Picha
Joseph Smith reading the scriptures
Picha
Church building with Church sign

Maneno Yesu Kristo ni sehemu muhimu sana ya jina la Kanisa. Kwa vile ni Kanisa la Yesu Kristo, limeitwa kwa jina Lake.

Picha
children holding scriptures

Watakatifu wa Siku za Mwisho humaanisha waumini wa Kanisa leo.

Picha
boy and grandma watching conference together

Manabii na mitume wamefundisha kwamba kutumia jina sahihi la Kanisa ni muhimu. Huwasaidia wengine kujua tunaamini katika Yesu Kristo.

Picha
girl showing friend picture of Jesus at home

Wakati wengine wanaponiuliza ninaamini nini, mimi husema, “Ninaamini katika Yesu Kristo, Mimi ni wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.”

Vielelezo na Apryl Stott

Chapisha