2021
Olga Šnederfler
Septemba 2021


Waanzilishi katika Kila Nchi

Olga Šnederfler

Matroni wa Kwanza wa Hekalu kutoka Czechoslovakia

Olga alijua kuwa angekwenda hekaluni siku moja.

Picha
woman sitting on chair looking at temple pictures

Olga alitazama picha ya hekalu ilyotundikwa kwenye ukuta wake. Alivuta pumzi. Kama tu familia yake ingekwenda hekaluni! Lakini hapakuwa na hekalu karibu, na ilikuwa vigumu pia kutoka katika nchi yake.

Olga alikuwa amebatizwa miaka mingi mapema. Lakini kisha wamisionari walilazimika kuondoka kutoka katika nchi. Waumini wa Kanisa hawakuruhusiwa kwenda kanisani tena. Hawangeweza kuzungumza na wengine kuhusu imani yao.

Olga aliendelea kuishi injili. Vile vile mumewe, Jiri. Waliomba na kusoma maandiko. Walikuwa na jioni ya nyumbani na kuwafundisha watoto wao. Jumapili, walikuwa na mkutano wa sakramenti katika nyumba yao ndogo. Walitundika picha nyingi za mahekalu.

Na wakati Olga na familia yake walipojisikia wapweke, walikumbuka kwamba kulikuwa na maelfu ya waumini wa Kanisa kote ulimwenguni.

Siku moja kitu cha kusisimua kilitokea. Rais Russell M. Nelson, Rais Mkuu wa Shule ya Jumapili, alizuru katika nchi yao. Olga alitabasamu wakati akipeana mkono na Rais Nelson. Kisha alimpatia ahadi maalumu. “Dada, siku moja wewe utakuja hekaluni.

Olga akasikia moyo umechangamka. “Asante,” alinong’ona.

Miezi ikapita. Kisha miaka. Olga alitazama huku akitamani picha za hekalu zilizotundikwa kwenye kuta. Kwenda hekaluni ilionekana kutowezekana!

Baada ya miaka minne, Olga na Jiri walialikwa kwenda kwenye mkutano mkuu Jijini Salt Lake, Utah, Marekani. Olga alikuwa na wasiwasi hawangeweza kwenda. Mambo katika nchi yao yalikuwa bado ni magumu. Ingewachukuwa kujaza fomu nyingi za usafiri. Lakini kwa njia fulani kila kitu kilienda vizuri. Olga alisikia vipepeo vikirukaruka tumboni mwake wakati ndege yao ilipoondoka kuelekea Marekani. Ilikuwa ni muujiza.

Olga na Jiri walienda kwenye mkutano mkuu na kumsikiliza nabii. Waliweza kuona Temple Square na kwenda kwenye kituo cha wageni. Lakini sehemu bora zaidi ilikuwa ni kuingia ndani ya hekalu.”

Wamevalia nguo nyeupe, Olga alijisikia kama vile alikuwa mbinguni alipokuwa anafanya maagano maalumu na Mungu. Hata aliunganishwa na Jiri. Ahadi ya Rais Nelson ikawa kweli!

Olga na Jiri walirudi nyumbani. Na wakati ukapita, mambo yakawa mazuri katika nchi yao Hatimaye waliweza kwenda kanisani, na wamisionari wangeweza kufundisha tena.

Siku moja simu ikalia. Ilikuwa ni Rais Thomas S. Monson. Alimpatia wito Olga kuwa matroni wa Hekalu la Freiberg Ujerumani. Jiri angekuwa rais wa hekalu.

Olga alitabasamu aliposimama katika vazi lake refu, jeupe ndani ya Hekalu la Freiberg. Hekalu lililoonekana wakati fulani kuwa mbali sana. Lakini sasa angeweza kulithamini kila siku! Ilikuwa ndoto ya ajabu kuwa kweli.

Eneo aliyoishi Olga baadaye lilikuja kuwa sehemu ya Jamhuri ya Czech.

Huko kuna mamia ya makasri katika Jamhuri ya Czech.

Matroni wa hekalu ni kiongozi wa kike katika hekalu.

Olga alikuwa na zaidi ya picha 20 za mahekalu nyumbani kwake.

Yeye na Jiri walikuwa na mvulana mmoja na binti mmoja.

Alikitunza kitabu chenye picha za wamisionari waliomfundisha.

Picha
Friend Magazine, 2021/09-10 Sep/Oct Tier 2

Vielelezo na Shawna J. C. Tenney

Chapisha