2021
Amigo Wapya
Septemba 2021


Amigo Wapya

Mwandishi anaishi Utah, Marekani.

Brigit hakuwa anajua Kihispania. Je, anaweza kukutana na mtu ye yote?

“Nalikuwa mgeni, mkanikaribisha” (Mathayo 25:35).

family driving car through street in Caracas

Brigit alitazama nje ya dirishani la gari wakati familia yake alipopitia katika mitaa myembamba ya Caracas, Venezuela. Kulikuwa na nyumba zenye rangi angavu na milima mikubwa ya kijani kibichi. Palikuwa mahali pazuri sana. Mama na baba walisema kuishi hapa lingekuwa tukio lisilo la kawaida.

Lakini Brigit bado alijisikia hofu. Leo ilikuwa ni mara yao ya kwanza kwenda kanisani katika nchi yao mpya.

Mama alimgekia Brigit. “Uko SAWA kipenzi?” aliuliza. “Hauonekani kama unajisikia vizuri sana.”

Brigit aligeuzageuza mikono yake. “Mie naogopa. Siwezi kuongea Kihispania. “Ninawezaje kupata rafiki?”

Mama akamsogelea na kuushika mkono wa Brigit. “Mimi najua una hofu. Lakini itakuwa SAWA. Vuta pumzi ndefu.”

Brigit alitazama chini kwenye mikono yake. Ilikuwa baridi, licha ya kuwa kulikuwa joto kali huko nje. Moyo wake ulikuwa unapiga kwa kasi, na akajisikia mvuvumko tumboni gari liliposimama kwenye sehemu ya maegesho ya kanisa. Kanisa lingekuwaje? Je, angeelewa cho chote?

Akitembea kuingia kanisani, Brigit alijiona mgeni. Alitazama kuzunguka familia zingine, wote wakiongea Kihispania. Kisha akaona wasichana wawili ambao walionekana karibia umri wake.

Punde wasichana walipomuona Brigit, walimkimbilia pale alipokuwa. Waliongea haraha haraka kwa sauti za furaha, na tabasamu kubwa.

Lakini hakuelewa cho chote walichosema. Wataenda zao wakigundua siwezi kuongea Kihispania? alijiuliza.

Brigit alivuta pumzi ndefu. “No hablo español,” alisema, huku akitingisha kichwa chake. “Siwezi kuongea Kihispania.” Machozi yakaanza kulengalenga machoni mwake.

Wasichana waliinua mabega yao na kutabasamu hata zaidi. Msichana mmoja akajinyoshea kidole na kusema, “Dayana.” Kisha akamuonyesha kidole yule mwingine na kusema, “Andrea.”

Hofu ya Brigit ikaanza kuyeyuka. Akarudisha tabasamu kwa wale wasichana na kujinyoshea kidole yeye mwenyewe. “Brigit.”

Dayana na Andrea wakakaa chini karibu na Brigit. Wakamfundisha jinsi ya kusema “maandiko” kwa Kihispania na maneno mengine machache. Wakati mkutano wa sakramenti ulipoanza, Moyo wa Brigit ulijisikia furaha na amani.

Baada ya Msingi, Brigit na marafiki zake wapya walikaa nyasini nje ya kanisa wakati wazazi wao wakiongea. Dayana na Andrea walimfundisha Brigit maneno zaidi ya Kihispania. Kisha Dayana akanyosha kidole kwenye mti na kuuliza, “¿Inglés?”

three girls sitting under palm tree

Brigit akatabasamu na kuonyesha kidole pia. “Mti,” alisema. Akachangamka na kuonyesha kidole kwenye vitu vingine, akisema maneno katika Kiingereza. Dayana na Andrea wakarudia maneno yale ya Kiingereza. Kisha wakamfundisha Brigit jinsi ya kuyasema kwa Kihispania. Brigit alijifundisha maneno ya aina zote yenye msaada, kama vile libro (kitabu), casa (nyumba), na coche (gari). Cha muhimu kabisa, walimfundisha jinsi ya kusema amigos (marafiki).

Punde ikawa wakati wa kwenda nyumbani. Brigit aliwapungia mkono wa kwa heri Dayana na Andrea.

“Imekuaje siku yako ya kwanza kanisani Venezuela?” Baba aliuliza.

Brigit alitabasamu. “Ilikuwa nzuri! Nimepata marafiki kadhaa. Na wananifundisha Kihispania!”

“Hiyo ni vizuri! Ninafurahi umekuwa na silu nzuri,”

Brigit alifikiria kuhusu jinsi Dayana na Andrea walivyomkaribisha. Hakujisikia kama mgeni tena. Alijua kwamba Baba wa Mbinguni alikuwa anamsaidia kupata marafiki. Na akawa na hamu ya kuona kile ambacho muda uliosalia katika Caracas ungekileta!

Friend Magazine, 2021/09-10 Sep/Oct Tier 2

Kielelezo na Julia Castaño