2021
Yesu Alisaidia katika Njia Nyingi
Septemba 2021


Kusaidia Kama Yesu

Yesu Alisaidia katika Njia Nyingi

Picha
Jesus helping a woman

Yesu alitumia maisha Yake akihudumu na kuwafundisha wengine. Wakati Yesu alipokuwa mdogo, Yeye alimsaidia baba Yake katika kazi ya useremala. Mmoja wa miujiza Yake ya kwanza ilikuwa ni kumsaidia mama Yake wakati mvinyo ulipoisha harusini. Wakati Yeye alipomwona mtu mwenye ulemavu wa macho, Yeye alimponya. Yeye aliwasaidia watoto kujisikia wanapendwa na kujumuishwa. Yawezekana sisi tusifanye miujiza ile ile Yesu aliyofanya, lakini tunaweza kufuata mfano wa Yesu kwa kutafuta njia za kusaidia katika njia bora tunayoweza.

Picha
Elierys decorating cookies

Mimi napenda kusaidia jikoni ili kutengeneza mapishi. Mimi napenda wanyama, na hiyo ndiyo sababu ninapenda kumsaidia babu yangu kuwalisha. Hivyo ndivyo ninavyosaidia!

Elierys R., umri miaka 9, Puerto Rico

Chapisha