Onyesha na Useme
Ilikuwa vigumu kusikiliza na kuwa na staha wakati tulipokuwa na kanisa nyumbani wakati wa janga la ulimwengu. Nilijaribu kufikiria jinsi ambavyo ningeweza kusaidia kufanya iwe maalumu na ya staha. Nilipata wazo. Nilichukua maboksi mawili makubwa na kuyatengeneza kuwa jukwaa. Nilisikia furaha kusaidia kufanya kanisa yetu ya nyumbani kuonekana kuwa maalumu.
Presley F., umri miaka 9, Saxony, Ujerumani
Ninapomuona mtu shuleni ambaye ni mpweke au ana wakati mgumu, huwaalika kucheza nami.
Otilia H., umri miaka 9, Region Hovedstaden, Denmark
Ninashukuru kwa ajili ya nabii aliye hai. Nafurahia kujifunza maandiko pamoja na familia yangu kila wiki tukitumia Njoo, Unifuate. Inanisaidia kuelewa mafundisho ya Yesu.
Cannon A., umri miaka 10, Arizona, Marekani
Nilikuwa nikisoma Kitabu cha Mormoni baada ya kuwa katika taabu. Mama yangu alikuja ndani na kuniona nikisoma na akasema ni wazo zuri la kunisaidia kutulia. Nilijisikia vizuri.
Ellie K., umri miaka 7, New Hampshire, Marekani
Nilipokuwa mgonjwa, nilihisi Roho Mtakatifu wakati baba yangu aliponipatia baraka za ukuhani. Ninashukuru kwa ajili ya mama na baba yangu.
Everett O., umri miaka 6, Ohio, Marekani
Ninaye gongola wa kufuga, na anapotoroka nasali kwa Baba wa Mbinguni nikiomba kwamba apate kurudi.
Ana C., umri miaka 6, Espírito Santo, Brazili
Rafiki yangu aliniomba kucheza mchezo wa video siku ya Jumapili. Kwa kweli nilitaka lakini nikasema hapana. Ninataka kuishika kitakatifu siku ya Sabato.
Benjamin C., umri miaka 9, California, Marekani
“Sisi Wote ni Wa”, Madison D., umri 10, Utah, Marekani
Alan M., umri miaka 10, California, Marekani
Dallin H., umri miaka 6, Auckland, New Zealand
“Hekalu,” Vimbai M., umri miaka 9, Dar es Salaam, Tanzania