2021
Kutana na Porter kutoka Poland
Septemba 2021


Mikono Saidizi Ulimwenguni Kote

Kutana na Porter kutoka Poland

Kutoka kwenye mahojiano na Amie Jane Leavitt.

Kutana na watoto wa Msingi wakiwasaidia wengine, kama Yesu alivyofanya.

Picha
two brothers sitting together

Yote kuhusu Porter

Umri: miaka 10

Kutoka: Marekani na anaishi Poland.

Lugha: Kiingereza na anajifunza Kifaransa

Familia: Baba, Mama, kaka Ethan, Mason, na Connor, na mbwa anayeitwa Ginger.

Malengo na ndoto: Kuwa daktari wa wanyama na kuwatunza wanyama.

Mikono Saidizi ya Porter

Picha
boy taking pictures at cemetery

Porter daima anatafuta mambo madogo madogo anayoweza kufanya ili kuwasaidia wengine. Nyumbani, huwasaidia wazazi wake kuaanda chakula kwa ajili ya familia. Shuleni, huhakikisha kila mtu anajumuishwa katika michezo, hasa watoto wale ambao kila mara wanasahaulika. Yeye husaidia kutunza vyombo vya wakati wa mapumziko, hata kama hakuvichezea yeye. Yeye pia hufanya mambo ya kuwasaidia wanyama. Yeye ni sehemu ya chama shuleni ambacho hutengeneza wanasesere kwa ajili ya mbwa kwenye makazi ya wanyama.

Porter pia alisaidia kwa kushiriki katika mradi wa BillionGraves. Yeye na familia yake walienda makaburini kupiga picha za mawe ya kichwani mwa makaburi. Kaka yake Connor alisaidia kupiga picha. Kisha walizipakia picha hizo kwenye tovuti ya mradi. Picha hizi zitawasaidia watu kote ulimwenguni ambao wanatafuta taarifa za mababu zao wa Kipolishi.

Mambo Ayapendayo Porter

Picha
pictures of Porter’s favorites

Mahali: Virginia, Marekani, na Herseypark katika Pennsylvania, Marekani.

Hadithi kuhusu Yesu: Wakati alipotuliza bahari.

Wimbo wa Msingi: “Gethsemane” (Machi 2018 Friend au Liahona)

Chakula: Mandoo (maandazi ya kinyunya ya Kikorea)

Rangi: Zambarau

Masomo Shuleni: Kusoma na hisabati

Porter akisaidia kupiga picha kaburini kwa ajili ya mradi wa ulimwenguni kote wa historia ya familia.

Chapisha