2021
Kadi za Historia ya Kanisa
Septemba 2021


Kadi za Historia ya Kanisa

Kata kadi, zikunje kwa kufuata mistari ya nukta kisha zifunge kwa kuzigundisha.

Desideria Yáñez

Picha
cut-out card of Desideria Yáñez

1814–1893

“Alikuwa na … hamu ya kusoma Kitabu cha Mormoni.”

  • Alipata ndoto kuhusu kipeperushi cha Kanisa ambacho kingebadilisha maisha yake.

  • Mwanawe, José, alikipata kipeperushi hicho katika Mji wa Mexico. Wamisionari walimfundisha injili.

  • Alikuwa mtu wa kwanza kusoma Kitabu cha Mormoni katika Kihispania.

  • Alikuwa mmoja wa wanawake wa kwanza kubatizwa katika Mexico.

Olivas Vila Aoy

Picha
cut-out card of Olivas Vila Aoy

1823–1895

Mimi … ningetamani kuwa mwenye usaidizi katika Kanisa.”

  • Alizaliwa Uhispania. Alisafiri hadi Cuba, Mexico, na Marekani kusaidia watu.

  • Alikutana na wamisonari na kujiunga na Kanisa.

  • Alisaidia kutafsiri Kitabu cha Mormoni kwa Kihispania.

  • Alipata kujua kwamba hakukuwa na shule za watoto ambao walikuwa wanaongea Kihispania katika EL Paso, Texas, Marekani. Kwa hiyo alianzisha shule kwa ajili yao na kufundisha kwa miaka mingi.

Vielelezo na Brooke Smart

Chapisha