Kutoka kwa Urais wa Kwanza
Kumwimbia Yesu
Imetoholewa kutoka “Kuabudu kwa njia ya Muziki,” Ensign, Nov. 1994, 9–12.
Kuimba nyimbo za dini na nyimbo za Msingi ni njia ya kuonesha upendo wetu kwa Yesu. Yeye aliweka mfano kwa ajili yetu. Mwishoni wa Chakula cha Mwisho, Yesu na Mitume Wake waliimba pamoja (ona Mathayo 26:30).
Kuimba kunaweza:
-
Kuonyesha upendo wetu kwa Yesu.
-
Kumleta Roho Mtakatifu.
-
Hutuandaa kujifundisha injili.
-
Kutupatia nguvu za kiroho.
Wakati unapoimba, fikiria kuhusu kile ambacho maneno yanasema. Wakati unapojaribiwa kufanya maamuzi mabaya, jaribu kuimba kimya kimya wimbo wa Msingi. Unapoimba, utajisikia kuwa karibu zaidi na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.
Amani katika Kristo
Usiku mmoja wakati Yesu na wanafunzi Wake wakiwa katika mashua kulikuwa na dhoruba kubwa. Wanafunzi waliogopa. Walimwamsha Yesu na kumuomba msaada. “Na [Yesu] aliamka na kuukemea upepo na kuiambia bahari Nyamaza, utulie. Na upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.” Marko 4:39
Paka rangi picha. Kisha andika chini baadhi ya nyimbo zako pendwa kuhusu Yesu. Unapojisikia kuwa mpweke au kuogopa, imba mojawapo ya nyimbo za kuleta faraja na amani.