2021
Hekalu la Kirtland
Septemba 2021


Hadithi za Maandiko

Hekalu la Kirtland

Picha
Joseph Smith seeing image of Kirtland Temple

Mungu alimwambia Joseph Smith ajenge hekalu. Lingekuwa nyumba ya Mungu.

Picha
children bringing water to workers building the temple

Watakatifu walifanya kazi kwa pamoja ili kusaidia kujenga hekalu hilo. Wanaume walijenga kuta ndefu. Wanawake walitengeneza mapazia na mazulia. Watoto walisaidia kuleta vifaa na maji kwa wanafanya kazi.

Picha
family singing together

Wakati hekalu lilipokamilika, Watakatifu waliingia ndani. Wao waliimba wimbo na kusema kwa sauti kubwa “Hosana!” Joseph alisema maombi ya kuweka wakfu (kubariki) hekalu.

Picha
Jesus appearing to Joseph and Oliver inside temple

Wiki moja baadaye, Yesu Kristo aliwatembelea Joseph Smith na Oliver Cowdery hekaluni. Yesu alisema Yeye amelikubali hekalu kama nyumba Yake.

Picha
three children holding hands and standing outside temple

Leo kuna mahekalu kote ulimwenguni! Kila hekalu ni mahali patakatifu. Siku moja mimi nitaenda ndani yake na kufanya maagano na Mungu.

Vielelezo na Apryl Stott

Chapisha