2023
Shughuli za Njoo, Unifuate
Januari 2023


Shughuli za Njoo, Unifuate

Kwa ajili ya jioni ya nyumbani, kujifunza maandiko au burudani tu!

Hakuna Kitu Kisichowezekana!

Picha
Hand with the middle finger bent down

Kwa ajili ya Mathayo 1; Luka 1

Hadithi: Elisabeti na Zakaria walikuwa wanataka kupata mtoto, lakini Elisabeti alilkuwa amezeeka sana. Siku moja, malaika alimtokea Zakaria na kumwambia kwamba wangepata mwana! Mwana wao alikuwa Yohana Mbatizaji. Elisabeti na Zakaria walijifunza kwamba kwa Mungu hakuna kitu kisichowezekana. (Ona Luka 1:11–14, 37.)

Wimbo: “A Child’s Prayer” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,12–13).

Shughuli: Jaribu hii kazi “Isiyowezekana”! Kwanza, kunja kidole chako cha kati. Kisha weka mkono wako mezani, kiganja kikiangalia chini. Sasa jaribu kuinua chanda cha pete. Kisha muombe mtu mwingine akuinulie. Je, ni kwa jinsi gani Baba wa Mbinguni amekusaidia kufanya kitu kilichoonekana kuwa hakiwezekani?

Hadithi ya Kuzaliwa kwa Yesu

Picha
Boy holding up baby book

Kwa ajili ya Mathayo 2; Luka 2

Hadithi: Kristo alizaliwa kwenye zizi katika mji wa Bethlehemu. Wachungaji, malaika na Mamajusi walikuja kumuona. Unaweza kusoma zaidi kuhusu Mamajusi kwenye ukurasa wa 46.

Wimbo: “Jesus Once Was a Little Child,” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 55)

Shughuli: Chukueni zamu kusimulia hadithi kuhusu kuzaliwa kwa mwanafamilia. Mnaweza kuzungumza kuhusu mahali walikozaliwa, lini walizaliwa, ni kina nani walikuwa wazazi wake au vitu vingine unavyovijua kuhusu kuzaliwa kwao.

Nuru ya Kweli

Picha
Girl shining a flashlight on the floor

Kwa ajili ya Yohana 1

Hadithi: Yesu Kristo wakati mwingine aliitwa “nuru ya kweli” (Yohana 1:9). Maandiko yanafundisha kwamba tunapaswa kutii amri Zake na kumfuata Yeye. Kisha tutapata “uwezo wa kuwa wana [na mabinti] wa Mungu” (Yohana 1:12).

Wimbo: “Jesus Is My True Light” (ukurasa wa 23)

Shughuli: Chora picha ya lengo ulilonalo. Acha mtu fulani afiche picha mahali fulani chumbani na uzime taa. Na sasa pata taa ndogo na umulike chumbani kote. Je, unaweza kupata picha yako sasa? Zungumza kuhusu jinsi Yesu Kristo anaweza kukusaidia kufikia malengo yako.

Njia ya Agano

Picha
Boy writing on paper

Kwa ajili ya Mathayo 3; Marko 1; Luka 3

Hadithi: Yesu Kristo alimwendea Yohana Mbatizaji kubatizwa ili “kutimiza haki yote” (Mathayo 3:15) Yesu alibatizwa ili kuonyesha mfano wa kumtii Baba wa Mbinguni. Tunaweza kumfuata Yesu kwa kubatizwa pia!

Wimbo: “Nifuate” (Nyimbo za Kanisa, na. 52)

Shughuli: Nenda kwenye ukurasa wa 9 ili ujifunze kuhusu njia ya agano. Kisha fanya shughuli. Kwenye ukurasa huu kila mwezi, utajifunza kuhusu baraka kwa ajili yako unapofuata njia ya kurudi kwa Baba wa Mbinguni!

Kielelezo na Katy Dockrill

Chapisha