Halo kutoka Uingereza!
Jifunze kuhusu watoto wa Baba wa Mbinguni duniani kote.
Uingereza ni nchi katika Ulaya Magharibi. Ni sehemu ya Ufalme wa Muungano wa Britania. Zaidi watu milioni 50 wanaishi huko.
Waanzilishi wa Mapema
Wamisionari wa kwanza walikuja Uingereza mnamo 1837. Watu wengi walibatizwa na kusafiri hadi Marekani. Sasa kuna karibia waumini wa Kanisa 150,000 katika Uingereza.
Lugha ya Kiingereza
Mwandishi William Shakespeare alitokea Uingereza. Alitunga mamia ya maneno ya Kiingereza. Leo watu bilioni 1.5 wanaongea Kiingereza.
Nyumba ya Kifalme
Uingereza ina mamia ya kasri. Kasri la Windsor lilijengwa katika karne ya 11 na ndilo kasri la zamani sana ambalo watu wanaishi ndani yake.
Usafiri katika London
London, Uingereza, ndiyo mji mkuu wa UK na ni mojawapo ya miji mikuu katika Ulaya. Una mabasi mengi marefu ya kusaidia watu katika usafiri.
Mahekalu Mawili Mazuri
Uingereza ina mahekalu katika Preston na katika London.