2023
Shughuli za Njoo, Unifuate kwa ajili ya Watoto Wadogo
Januari 2023


Agano Jipya

Shughuli za Njoo, Unifuate kwa ajili ya Watoto Wadogo

Picha
A brother and sister play with sticks and dead grass while playing outside.

Kwa ajili ya Mathayo 1; Luka 1

Elezea kwamba Agano Jipya ni kuhusu Yesu. Tunajifunza jina Lake katika sura ya kwanza (ona Mathayo 1:21). Andika maneno Yesu Kristo kwenye kipande cha karatasi na kumpa mtoto wako bidhaa za sanaa za kuremba karatasi hilo!

Kwa ajili ya Mathayo 2; Luka 2

Onyesha picha ya mandhari ya Kuzaliwa ikiwa na Yesu, Mariamu na Yusufu. Eleza kwamba Yesu wakati mmoja alikuwa mtoto pia. Waambie kwamba wazazi Wake walimpenda Yeye sana—kama vile unavyowapenda wao. Wakumbatie watoto wako wadogo na uwaambie kile unachowapendea.

Kwa ajili ya Yohana 1

Wapeleke watoto wako wadogo kwa matembezi ya nje. Tazama nao vitu vya kuvutia katika mazingira asili—kama vile miti, ndege, upepo au anga. Waache watoto wako watwae mawe au wanuse maua. Waambie, “Yesu anawapenda na aliumba ulimwengu huu mzuri kwa ajili yenu.”

Kwa ajili ya Mathayo 3; Marko 1; Luka 3

Imba “When Jesus Christ Was Baptized” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 102). Elezea kwamba Yesu alibatizwa ili kumtii Baba wa Mbinguni. Siku moja, watoto wako wadogo wanaweza kuchagua kubatizwa pia! Waambie watoto wako kuhusu ubatizo wako. Kwa nini ulikuwa maalumu kwako?

Chapisha