Kelele Nyingi Mno!
Kila kitu kilikuwa na kelele nyingi sana. Ni wapi ambapo Luke angeweza kupata amani?
Luke aliguna. Kila kitu kilikuwa na kelele nyingi mno. Kaka zake, Tadd na John, walikuwa wanabishana tena. Hata kutoka barazani, angeweza kusikia makelele yao kupitia mlango wa chumba chao. Na dada yake, Lizzie, alikuwa ameweka muziki sauti ya juu sana tena. Dunda. Dunda. Dunda. Yeye angeweza daima kusikia mdundo imara wa noti za chini.
Luke alijaribu kuwaomba kaka zake kusitisha. “Nenda zako,” Tadd alimwambia. Kisha Luke akamwomba Lizzie apunguze sauti ya muziki. Naye Lizzie akaongoze sauti ya muziki sana.
Luke alitaka kwenda nje ambapo angeweza kufikiria. Lakini mvua ilikuwa inanyesha.
Kulikuwa na sehemu ya ukimya ambako Luke angeweza kwenda. Jana wazazi wake walimpatia yeye chumba chake mwenyewe—ambacho yeye hakuhitajika kutumia pamoja na Tadd na John. Ilikuwa ni sehemu ya chumba kilicho chini ya ardhi. Kilikuwa kikubwa kutosha kitanda na meza. Lakini katika chumba chake Luke angeweza kufunga mlango na kuepuka kelele.
Luke alishuka ngazi kwenda katika chumba chake kipya. Alitazama huku na huku kwenye maboksi aliyoyaleta kwenye chumba. Aliona picha ya Yesu ikitokeza kwenye boksi mojawapo. Luke alikuwa amepata picha hii katika siku aliyobatizwa. Mara zote alipokuwa akiitazama ilimfanya kuhisi amani.
Luke aliitoa picha hiyo kutoka kwenye boksi. Aliiweka kwenye meza. Kisha alipiga magoti kusali. “Baba wa Mbinguni,” Luke alisema, “wakati mwingine hapa kuna kelele sana. Tafadhali nisaidie nipata amani.”
Luke akajilaza kitandani pake. Akafikiria kuhusu Yesu. Alijifunza katika Msingi kwamba Yesu angekuwa karibu naye daima. Na Roho Mtakatifu daima angemletea amani.
Punde Mama na Baba wangefika nyumbani kutoka kazini. Wangezungumza na Tadd na John. Vita vingekoma. Katika muda mfupi. Wangezungumza na Lizzie. Lizzie angepunguza sauti ya muziki wake. Katika muda mfupi. Mpaka Mama na Baba watakapoondoka tena.
Lakini kwa sasa, Luke alijilaza kitandani. Aliitazama picha ya Yesu. “Tafadhali, Baba wa Mbinguni,” Luke alinong’ona. “Tafadhali nisaidie kuhisi amani bila kujali kile kinachoendelea hapa nyumbani.”
Baadaye, mlango wa chumba chake ulibishwa. “Naomba kuingia ndani?” Mama aliomba. “Unaendeleaje?”
“Tadd na John walikuwa wanapigana tena,” Luke alisema. “Na lizzie alicheza muziki kwa sauti kubwa sana.”
“Ninajua. “Ni vigumu, si ndio?” Mama alisema. “Baba yako anazungumza na kaka zako saa hii. Nami nitazungumza na Lizzie usiku wa leo. Lakini kwanza, ningependa kujua unaendeleaje.”
“Mimi niko SAWA. Nashukuru nina chumba hiki,” Luke alisema.
“Mimi pia,” Mama alisema. “Naona umeweka picha ya Yesu mezani.”
Luke alitabasamu. “Nimefanya hivyo. Na Yeye atanisaidia kufanya chumba changu kuwa mahali pa amani.”