2023
Kutambua Talanta Zangu
Januari 2023


Watoto na Vijana

Kupata Talanta Zako

Picha
A young boy smiles as he looks up at a bird that is in a tree. He is holding a book about birds.

Nilipoanza kuweka malengo kwa ajili ya Watoto na Vijana, mimi pamoja na mama yangu tulizungumza kuhusu ni talanta zipi mpya ningetaka kujifunza. Nilitaka kufanya mazoezi ya kuimba, kudensi na kucheza kinanda. Pia nilitaka kujifunza kuhusu wanyama na nilitaka kujifunza kupika. Pia nilitaka kusoma Kitabu cha Mormoni!

Mama yangu alinifunza vitu vingi kuhusu kukuza talanta zangu. Mwanzoni ilikuwa ngumu. Lakini nilifanya mazoezi zaidi na zaidi. Sasa ninaweza kucheza “Mimi ni Mtoto wa Mungu,” “Do, Re, Mi,” na “Mary Had a Little Lamb” kwenye kinanda. Nilijifunza jinsi ya kupika wali na soseji katika mkate na jinsi ya kuoka biskuti. Nilisoma baadhi ya vitabu kuhusu wanyama. Sasa ninajua majina ya ndege wengi, kama vile ndege mwenye rangi nyingi, keremkeremu na koleamiti. Na niliweza kumaliza kusoma Kitabu cha Mormoni kabla ya kufika miaka tisa. Ilikuwa vyema kumaliza kitabu chote baada ya miaka miwili.

Natumaini watoto wengine wa Msingi watajifunza zaidi kuhusu Yesu Kristo na talanta walizonazo.

Kielelezo na Kylah Garcia

Chapisha