Jinsi Siedeh Alivyokuwa Jasiri
Siedeh alikuwa anaogopa sana kuzungumza na wanadarasa wenzake.
Siedeh alivuta pumzi kubwa na kutembea katika darasa lake jipya. Ilikuwa ni siku yake ya kwanza katika darasa la nne.
Mwaka jana, Siedeh alikuwa darasa la pili. Alifanya vyema sana mpaka shule yake ilimruhusu kuruka darasa la tatu. Siedeh alikuwa na msisimko wa kufanya hisabati ngumu na kusoma vitabu vingi katika darasa la nne. Lakini hakuwa na furaha kwamba angewaacha marafiki zake wa zamani.
Alipokuwa akitazama darasa lake, Siedeh alihisi kuwa mdogo. Wote kati ya wanadarasa wenzake wapya walionekana kuwa wakubwa na warefu kuliko vile alivyokuwa. Itakuwaje kama atahisi kutokuwa sehemu yao?
Kisha alichagua dawati na kuketi. Msichana mrefu aliketi karibu naye. “Halo,” Siedeh alisema.
“Unafanya nini hapa?” msichana aliuliza. “Mimi nilidhani unapaswa kuwa darasa la tatu.”
“Shule imenisogeza juu darasa moja,” Siedeh alisema kwa uoga.
Msichana yule akakunja uso. “Vyema, mimi sijali jinsi wewe ulivyo mwerevu. Wewe bado ni mtoto mchanga.”
Siedeh alihisi vibaya sana. Kwa wiki yote, alikuwa anaogopa sana kuzungumza na yeyote wa wanadarasa wake. Kila wakati yeye alipomsikia mtu akicheka au akinong’ona, alinuna. Huenda walikuwa wakisema vitu vibaya kumhusu yeye.
Alipofikiria kwamba mambo hayatakuwa mabaya zaidi, Siedeh alipata majibu ya mtihani wa hisabati. Alitaka kulia wakati alipotazama maksi yake. Hisabati lilikuwa somo lake pendwa. Kamwe hajawahi kupata maksi kidogo kama hayo kwenye mtihani hapo awali.
Wakati alipofika nyumbani, Siedeh hakuweza kuzia machozi yake. “Sina marafiki kabisa,” aliwaambia wazazi wake. “Mimi si wa darasa la nne. “Mimi si mwerevu vya kutosha.”
“Pole imekuwa vigumu,” mama yake Siedeh alisema. “Lakini wewe ni mwerevu. Na bado unaendelea kujifunza.”
Siedeh akafuta macho yake. Natamani ningeenda darasa la tatu badala yake.”
Baba alikuwa kimya kwa muda. Je, ungependa kupata baraka ya ukuhani?” yeye aliuliza.
Siedeh aliitikia kwa kichwa. Labda baraka kutoka kwa Baba ingemsaidia kuhisi vizuri zaidi.
Siedeh aliketi, na Baba akamwekea mikono yake juu ya kichwa chake.
“Ninakubariki wewe kwamba hautakuwa na uoga,” Baba alisema. “Ninakubariki wewe uwapende wanadarasa wenzako wapya. “Na wanapokufahamu, watakupenda wewe pia.
Hisia za utulivu zikasambaa kwa Siedeh. Alihisi kwamba maneno ya baba yake yalikuwa kile Baba wa Mbinguni alitaka yeye asikie.
Baada ya kupokea baraka, Mama alimsaidia Siedeh na hisabati. Punde Siedeh akaaza kuhisi vyema kidogo.
Siku iliyofuata shuleni, Siedeh alikumbuka baraka yake na kujaribu kuwa jasiri. Alitabasamu kwa wanadarasa wenzake. Wakati alionyesha upendo, alihisi kutowaogopa sana! Baadhi yao walikuwa hata wazuri sana. Alifanya kazi kwa bidii kujifunza, na punde alama zake zikawa nzuri pia.
Kufikia mwisho wa mwaka wa shule, Siedeh akawa na marafiki wengi. Alikuwa na furaha kwamba Baba wa Mbinguni alikuwa amemsaidia kuwa jasiri. Na alikuwa na shukrani daima angekuwa na baraka za nguvu za ukuhani kumsaidia.