2023
Kusaidia Kazi ya Baba wa Mbinguni
Januari 2023


Rafiki kwa Rafiki

Kusaidia Kazi ya Baba wa Mbinguni

Kutoka kwenye mahojiano na Richard M. Romney.

Je, unajua umealikwa kumsaidia Baba wa Mbinguni katika kazi Yake muhimu? Kazi hiyo ni kuwasaidia watoto Wake wote kurudi na kuishi Naye (ona Musa 1:39). Unaweza kusaidia unapofanya vitu vinne: ishi, jali, alika, na unganisha.

Ishi injili ya Yesu Kristo. Unaishi injili unapofuata mfano wa Yesu. Unaweza kusali, kusoma maandiko au vitabu vya hadithi vya maandiko, kuwasamehe wengine na kuhudhuria kanisani.

Jali wale walio na mahitaji. Unaweza kuketi chini na mtu aliye mpweke. Au unaweza kuwa rafiki kwa watu wagonjwa na kuwachangamsha.

Waalike wote kuipokea injili. Unaweza kuwaalika marafiki kanisani au katika shughuli ya darasa la Msingi. Unaweza kuwaalika marafiki kwenye ubatizo wako.

Unganisha familia milele. Unaweza kuzungumza na mababu zako kujifunza kuhusu maisha yao. Unaweza kuwa mpatanishi katika nyumba yenu. Unaweza kujiandaa mwenyewe kwenda hekaluni

Ninawaahidi kwamba mtahisi furaha mnapojaribu kuishi, kujali, kualika na kuunganisha nyumbani, shuleni na katika Msingi. Baba wa Mbinguni anakupenda! Na wewe unaweza kusaidia katika kazi Yake muhimu.

Vielelezo na Augusto Zambonato

Chapisha