2023
Kumfuata Yesu huko Uingereza
Januari 2023


Kumfuata Yesu huko Uingereza

Kutana na Lucia, Vivie na Zac!

Kuwahusu Wao

Picha
Vivie and Lucia Jenkins (sisters) smile as they stand next to a miniature pony.
Picha
Zac Jenkins smiles as he stands next to a very tall sunflower.

Majina: Lucia, umri miaka 7; Vivie, umri miaka 9; na Zac, umri miaka 9

Kutoka: Herefordshire, Uingereza

Lugha: Kiingereza

Malengo na ndoto: Kuwa rafiki mwema (Lucia), kukariri Makala ya Imani (Vivie) na kuwasaidia watoto kucheza michezo (Zac)

Familia: Lucia na Zac ni kaka na dada na Vivie ni binamu yao.

Je, Ni kwa Namna Gani Wao Wanamfuata Yesu

Picha
Two boys pushing a lawn mower

“Familia zetu zinaishi kwenye shamba moja na Bibi na Babu,” Lucia anasema. “Kuna kazi nyingi za kufanya, lakini tunahisi vizuri wakati tunapotumikia. Tunajua kwamba Yesu Kristo anatutaka tutumikie.”

“Tunamsaidia Bibi kuwatunza farasi wadogo,” Vivie anasema. “Tunawaongoza kondeni kulisha. Tunasafisha zizi la farasi, kuchana manyoya yao, kuwalisha na kujaza ndoo zao za maji. Tunapenda kumsaidia Bibi.”

Zac humfuata Yesu kwa kutumikia pia. “Babu mkuu wetu alifanyiwa upasuaji kwenye mkono wake. Hangeweza kutunza bustani lake. Familia yangu, binamu, akina babu na bibi walisaidia kufyeka nyasi na kuondoa magugu. Babu mkuu alikuwa na furaha sana!”

Mapendeleo Yao

Picha
1. A map of Great Britain: With the Preston England Temple, London England Temple, and Icon landmarks around the country to create an England feel. The background would extend behind the blocks of type, see rough layout. The dimensions include the background. 2. An Envelope 3. Two girls, Lucia (age 7) and Vivie (age 9), riding horses together. 4. Collage of Mangos, Sweet potatoes, Broccoli 5. Queen Elizabeth 6. Three colored pencils: (Turquoise, purple and yellow)

Mahali: Lucia na Vivie wanapendelea kuwa na farasi

Hadithi ya Maandiko: Anachopenda Zac ni wakati Yesu alitembea juu ya maji

Tunda au mboga: Maembe (Lucia), viazi vitamu (Vivie), brokoli (Zac)

Rangi: Zambarau (Lucia), feruzi (Vivie) na njano (Zac)

Somo shuleni: Sanaa (Lucia na Vivie) na historia (Zac)

Chapisha