2023
Taa, Kamera, Huduma!
Januari 2023


Taa, Kamera, Huduma!

Kuwa nyumbani hakutuzuii kuhudumu.

Picha
“Lights, Camera, Service” is about two sisters who were sad they couldn’t go to church because of the COVID-19 pandemic – they decided to make videos in Spanish to help other kids. 1. A sad girl looking at the computer. 2. Two sisters talking and looking online for lesson ideas. 3. Two sisters taking turns recording themselves as they talk about stories in the Book of Mormon. 4. Spot of six primary kids on a computer zoom meeting and a text bubble coming up from one of the sisters talking about the stripling warriors story in the Book of Mormon.

Antonella na Mariana wanapenda kwenda kanisani kila wiki. Lakini sasa hawangeweza kwenda kanisa kwa sababu ya janga la UVIKO-19. Walikuwa na darasa la Msingi mtandaoni, lakini darasa halikuwa sawa na la kawaida.

Antonella na Mariana walitamani sana kuhudhuria Msingi uso kwa uso. Mwaka uliopita, familia yao ilihama kutoka Chile hadi Kanada. Janga lilifanya iwe vigumu kupata marafiki wapya. Walitamani sana kujifunza kuhusu hadithi za maandiko pamoja na watoto wengine. Na walitamani kuwa na masomo katika lugha ya Kihispania kama vile walivyofanya huko Chile.

Siku moja, baada ya kuwa na kanisa nyumbani, Antonella na Mariana walitafuta kitu fulani kuwasaidia kujifunza Njoo, Unifuate.

“Ninatamani ningepata video zaidi za Kihispania,” Antonella alisema. Alifikiria kwa muda mfupi. Kisha akapata wazo bora. “Tunaweza kutengeneza video zetu wenyewe za Njoo, Unifuate kila wiki.”

“Ndio, na tungeweza kuzitengeneza kwa Kihispania!” alisema Mariana. “Kisha tungeweza kuzishiriki na watoto wengine pia.”

Mamá na Papá walisema wangesaidia. Familia yote ilifurahia!

Kwanza familia ilisoma maandiko ya somo la wiki. Wasichana walipanga kile ambacho wangezungumza. Kisha walianza kutengeneza video. Antonella na Mariana walichukua zamu kujirekodi wenyewe walipokuwa wanazungumza kuhusu hadithi katika Kitabu cha Mormoni. Mwisho wa kila video, mmoja wao alishiriki kitu fulani walichojifunza kutoka kwenye somo. Kisha Mamá na Papá waliwasaidia kutengeneza video za kuweka mtandaoni.

Kwanza, walikuwa hawajui cha kusema. Lakini kusoma maandiko na kujifunza zaidi kuhusu masomo kuliwasaidia.

Jumapili moja, Antonella na Mariana walikaa mbele ya kompyuta kwa ajili ya darasa lao la Msingi. Somo la wiki hii lilikuwa kuhusu askari vijana katika Kitabu cha Mormoni. “Kwa nini askari vijana walienda vitani?” mwalimu aliuliza.

Mariana aliwasha kinasa sauti. “Najua,” akasema. Yeye na Antonella walikuwa wametengeneza video kuhusu hadithi hiyo wiki iliyopita. “Baba zao walimwahidi Mungu kwamba hawatapigana, kwa hiyo wana walienda vitani badala yao.”

Antonella aliitikia kwa kichwa. “Na mama zao waliwafunza kwamba kama wangekuwa na imani, Mungu angeweza kuwatunza wawe salama.” Alimtabasamia Mariana. Ilifurahisha kujifunza maandiko pamoja.

Usiku ule wakati wa chakula cha jioni, Mamá aliuliza, “Msingi ilikuwaje?”

“Vyema” Antonella alisema. “Kutengeneza video kumenisaidia kujifunza sana kuhusu maandiko.”

“Mimi pia!” alisema Mariana. “Ninaweza kujibu maswali mengi katika Msingi. Na ninajua hadithi za Maandiko vyema.”

“Nashukuru video zimewasaidia,” Papá alisema. “Ninafikiria zimesaidia watu wengine wengi pia!”

“Hiyo ni sawa,” Mamá alisema. “Kushiriki kile mlichojifunza na jinsi mnavyohisi kuhusu injili ni njia nzuri ya kuhudumu!”

Mariana alitabasamu. “Ninapenda kwamba tunaweza kutumikia kwa njia hii,” alisema. Kisha akamgeukia Antonella. “Acha tuanze kupanga juu ya video ya wiki ijayo!”

Chapisha