Kumwakilisha Yesu
David alikuwa na woga kupitisha sakramenti kwa mara ya kwanza.
David aliketi kwenye safu ya mbele ya kanisa dogo na kuchezesha mguu wake. Alikuwa akiogopa. Alikuwa tu ndio amehama toka Msingi na kuwa shemasi. Wavulana wakubwa walikuwa wanamwonyeshe David na wavulana wengine wa umri wa miaka 11 jinsi ya kupitisha sakramenti.
Ugonjwa wa akili wa watoto aliokuwa nao David wakati mwingine ulifanya iwe vigumu kwake kujifunza mambo mapya. Kutoka kwenye Msingi kumekuwa vigumu kwake. Na sana kupitisha sakramenti kulionekana kuwa kwa kuogofya. Vipi kama angefanya makosa na kila mtu amcheke?
Jacob, mmoja wa wavulana wakubwa, alikaa karibu na David. “Tunafurahi kuwa na wewe pamoja nasi,” Jacob alisema. Jacob akampa David salamu. “Utakuwa bora sana wewe.”
David alitabasamu. Hiyo ilimfanya kuhisi vyema kidogo.
Vijana wengine waliwaonyesha wavulana wa umri wa miaka 11 nini cha kufanya. Waliwaonyesha wapi pa kwenda na ni safu gani watapitisha. Walifanya zoezi la kutembea kwenye njia baina ya viti kanisani. Waliwaonyesha wavulana jinsi ya kushika trei za sakramenti.
“Mama, tazama!” David alisema alipokwenda nyumbani. Aliinua mkono wake juu. Hivi ndivyo jinsi ninashikilia trei. Kwa makini, hivi. Kwa sababu ninamwakilisha Yesu, na ninataka kuonyesha heshima zangu.”
Wavulana wakubwa walifanya zoezi pamoja na David na wavulana wengine siku za Jumapili baada ya ibada na wakati wa shughuli za wiki za usiku. Walitembea kupita pale walipohitajika kupita. David alifanya zoezi la kushikilia trei.
Punde, siku ikafika ambapo angepaswa kupitisha sakramenti kwa mara ya kwanza.
“Je, wewe unahisi vipi kuhusu hilo?” Baba aliuliza.
“Bado nina woga,” David alisema.
“Acha tupitie tena kile mlichofanya ili kujiandaa,” Baba alisema.
“Vyema, tulisoma maandiko kuhusu ukuhani kama familia,” David alisema. “Kushikilia ukuhani humaanisha kumwakilisha Yesu. Nilikata kucha zangu ili mikono yangu ionekana vizuri. Na nimefanya mazoezi sana!”
“Nafikiri unaoneka umejiandaa vyema,” Baba alisema.
Alipofika kanisani, David aliketi kwenye safu ya mbele pamoja na mashemasi wengine. Jacob aliketi karibu naye. David alifikiria kuhusu jinsi angemwakilisha Yesu wakati akipitisha sakramenti. Itakuwaje kama akikosea? David alimtazama Jacob na Jacob akamtabasamia. David alitabasamu na akavuta pumzi ndefu.
Wakati wa kupitisha sakramenti ulipofika, Jacob alimsaidia David kupitisha trei katika safu chache za kwanza. David alikuwa na furaha kwa kuwa na mtu akiwa pamoja naye.
David aliwatazama watu alipokuwa anapitisha sakramenti. Wengi wao walikuwa wameketi kama wameinamisha vichwa vyao kwa staha. Wengine walikuwa kwenye tafakuri. David alihisi amani. Alikuwa anamwakilisha Yesu. Alishukuru angeweza kuwasaidia wengine kufikiria kuhusu Yesu Kristo.