2021
Kazi Kuu: Wimbo wa Dhima ya Vijana kwa Mwaka 2021
Januari 2021

“Kazi Kuu: Wimbo wa Dhima ya Vijana kwa Mwaka 2021,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Januari 2021, 22–25.

Kazi Kuu

Wimbo wa Dhima ya Vijana kwa Mwaka 2021

Picha
Kazi Kuu: Wimbo wa Dhima ya Vijana kwa Mwaka 2021
Picha
Kazi Kuu: Wimbo wa Dhima ya Vijana kwa Mwaka 2021

Kuna kazi ya kufanya

iliyoandaliwa kwa ajili yako

zamani kabla ya ulimwengu kuumbwa.

Unayo nguvu unayohitaji

kuvuka bahari zenye dhoruba

utakazokutana nazo njiani.

Yeye ni kimbilio lako kwenye dhoruba.

Na kamwe hutakuwa pekee yako.

Hii ni kazi kuu ambayo tumepewa.

Hii ni sehemu ya mpango Wake mkuu.

Hivyo usichoke. Yeye atakuwa pamoja nawe,

Na atakuongoza usiku wote

katika kazi hii kuu. Kazi hii kuu. Hii ni kazi kuu.

Ikiwa utampa Yeye moyo wako,

Atakuonyesha kuwa wewe ni nani

na matumaini na ndoto Zake zote juu yako.

Na unapomfuata Yeye,

kazi hiyo kuu itaanza

na upendo mkamilifu utashinda.

Hii ndiyo kazi kuu ambayo tumepewa.

Hii ni sehemu ya mpango Wake mkuu.

Hivyo usichoke. Yeye atakuwa pamoja nawe,

Na atakuongoza usiku wote

katika kazi hii kuu. Kazi hii kuu. Hii ni kazi kuu.

Chapisha