“Jibu kwa ajili ya Oliver,” Kwa ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Januari 2021, 12–13. Njoo, Unifuate Jibu kwa ajili ya Oliver Imeandikwa na Eric B. Murdock, vielelezo na Lance Fry Oliver Cowdery alikuja kuishi nyumbani kwa Joseph Mkubwa na Lucy Mack Smith wakati alipokuwa akifundisha shule iliyokuwa karibu na shamba lao. Oliver alisikia kuhusu mwana wao Joseph na mabamba ya dhahabu. Alitaka kujua zaidi. Oliver alitamani kujua jinsi ambavyo Mungu alimpa Joseph uwezo wa kutafsiri mabamba hayo ya dhahabu. Nataka kusaidia katika kutafsiri. Mara shule itakapofungwa, nitakwenda kumsaidia Joseph. Unapaswa kumuomba na kumuuliza Bwana kama hilo ni sahihi kwako. Usiku huo Oliver aliomba na akamuuliza Bwana kile anachopaswa kufanya. Oliver alijisikia amani wakati alipoomba kuhusu kumsaidia Joseph kutafsiri. Haikupita muda mrefu Oliver alikwenda kukutana na Joseph Smith. Alisafiri pamoja na Samweli kaka wa Joseph. Joseph, nimekuja kukusaidia. Ninaweza kuwa mwandishi wako. Asante. Ninashukuru kwa usaidizi wako. Joseph na Oliver wakaanza kutafsiri. Jambo hili lilimsisimua Oliver, lakini bado alikuwa na maswali. Siku moja, Joseph alipokea ufunuo kwa ajili ya Oliver kumkumbusha kuhusu jibu la ombi lake. “ Amin, amin, ninakuambia, kama wataka ushahidi zaidi, rejesha mawazo yako juu ya usiku ule uliponililia katika moyo wako, kwamba uweze kujua ukweli wa mambo haya. “Sikusema amani akilini mwako kuhusiana na jambo hili? Ni ushahidi gani mkubwa zaidi unaoweza kupata kuliko kutoka kwa Mungu?”1 Niliomba ili kufahamu ikiwa napaswa kuja kukusaidia, nami nikajisikia amani. Hakuna ambaye angefahamu kuhusu hili isipokuwa Mungu. Oliver alijua kwa uhakika kuwa kazi ilikuwa ya kweli. Yeye na Joseph walikamilisha tafsiri ambayo ilikuja kuwa Kitabu cha Mormoni.