2021
Ujumbe Kutoka kwa Urais wa Kwanza
Januari 2021


“Ujumbe Kutoka kwa Urais wa Kwanza,” Kwa ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Januari 2021, 2.

Ujumbe Kutoka kwa Urais wa Kwanza

Wapendwa akina kaka na dada zetu vijana,

Tuna furaha kuwatambulisha kwenye jarida hili jipya la vijana wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho: Kwa ajili ya Nguvu Kwa Vijana. Tunashukuru kwa wema na uwezo wenu kama vijana wa Kanisa. Kweli ninyi ndio tumaini la Israeli. Ni tumaini letu la dhati kuwa chapisho hili jipya litawasaidia kubakia imara na karibu na Baba yenu wa Mbinguni na Mwokozi wetu, Yesu Kristo.

Bwana ana kazi kuu kwa ajili yako na kizazi chako. Ili kukusaidia, jarida hili litatoa mafundisho ya kukufaa kuhusu manabii na mitume wa siku za leo, ambao wanakupenda. Unaposoma maandiko ukitumia nyenzo za Njoo, Unifuate za Kanisa zinazokusaidia kuishi na kujifunza injili ya Yesu Kristo, unaweza pia kusoma jarida hili ili kupata ufahamu, utambuzi na uvuvio wa ziada.

Kwa mara ya kwanza, chapisho hili maalum linalojitegemea kwa ajili ya vijana, linapatikana katika nchi tofauti na kwa lugha tofauti. Tunatumaini kwamba hili litaleta roho ya kuwa sehemu ya ulimwengu wote na umoja na kwamba mtapata nguvu kutokana na shuhuda na uzoefu walioushiriki vijana wengine kutoka kote ulimwenguni.

Jina la jarida hili linaashiria kuwa tunaamini kwamba mna nguvu kama vijana wa Kanisa. Tunashuhudia kuwa furaha ya kweli huja kupitia imani yetu kwa Yesu Kristo, injili yake na Kanisa Lake lililorejeshwa.

Kwa Moyo wa Dhati,

Urais wa Kwanza

Chapisha