2021
Sehemu ya Burudani
Januari 2021


“Sehemu ya Burudani,” Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana, Jan. 2021, 28–29.

Sehemu ya Burudani

Picha
Sehemu ya Burudani

Imezama katika Hesabu

Watu wanaofanya ubatizo wanapaswa kusema maneno mahsusi. Maneno hayo yanapatikana kwenye Mafundisho na Maagano 20, lakini ni mstari gani? Fanya hesabu ifuatayo ukitumia nambari kutoka kwenye maandiko ili upate jibu.

  1. Chukua idadi ya sehemu zilizo kwenye kitabu cha Mafundisho na Maagano kisha utoe umri wa Joseph Smith alipopokea Ono la Kwanza (soma Joseph Smith—Historia ya 1:23).

  2. Chukua jibu la A na ligawanye kwa idadi ya vitabu vilivyo kwenye Kitabu cha Mormoni vinavyoitwa “Nefi.”

  3. Chukua jibu la B na kuzidisha mara idadi ya nyakati ambazo malaika Moroni alimtembelea Joseph Smith usiku wa Septemba 21–22, 1823 (soma Joseph Smith—Historia ya 1:30–47).

  4. Chukua jibu la C na ondoa idadi ya makabila ya Israeli (ona, kwa mfano, Mwanzo 49:28).

  5. Chukua jibu la D na ondoa umri ambao mtu akifika anaweza kubatizwa.

Majibu

Tambua Tofauti

Je, unaweza kutambua mambo 10 yaliyo tofauti kati ya picha hizi mbili?

Majibu

Vichekesho

Picha
mama na mwana

Roho anaweza kuwa kwenye mkono wako wa kulia na kushoto na malaika wanakuzingira, lakini bado umevalia helmeti!

Arie Van de Graaff

Picha
mama na binti

Asante kwa kunisaidia kuingiza ndani vyakula! Usiingilie tu biskuti. Hizo ni kwa ajili ya somo langu la Shule ya Jumapili!

Ryan Stoker

  1. Fanya Hesabu: A. 138-14=124 B. 124÷4=31 C. 31×3=93 D. 93-12=81 E. 81-8=73 Jibu: Mafundisho na Maagano 20:73

  2. Tambua Tofauti: 1. Ua limebadilika rangi. 2. Tai imebadilika rangi. 3. Hakuna mikanda. 4. Rangi ya tai ndogo imebadilika. 5. Hakuna mkufu. 6. Hakuna pesa kwenye mfuko wa shati. 7. Hakuna kitambaa cheupe cha kichwani. 8. Dasta ya manyoya imebadilika rangi. 9. Ukuta wa nyuma umebadilika rangi. 10. Gauni limebadilika rangi kwa msichana aliye katikati kwenye safu ya nyuma.

Chapisha