“Kujifunza Lugha ya Roho Mtakatifu,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Januari 2021, 16–18.
Njoo, Unifuate
Kujifunza Lugha ya Roho Mtakatifu
Ufunuo ni kama lugha ambayo kila mmoja wetu anapaswa kujifunza.
Kujifunza lugha mpya inaweza kuwa kazi ngumu. Kama umewahi kuhudhuria madarasa ya lugha shuleni au umejaribu kujifunza lugha mwenyewe, unaweza ukawa unafahamu hili kutokana na uzoefu! Inahitaji jitihada na kujitolea. Nilijifunza Kihispania nilipokuwa katika misheni yangu, ambayo mwanzoni ilikuwa vigumu, lakini hatimaye, kwa usaidizi wa Roho Mtakatifu Mtakatifu, nilifaulu.
Napenda kufikiria ufunuo kama lugha ya aina fulani—lugha ya Roho Mtakatifu—ambayo sote tunahitaji kujifunza maishani. Rais Russell M. Nelson alisema, “Katika siku zijazo, haitawezekana kuendelea kuishi kiRoho Mtakatifu bila mwongozo, maelekezo, faraja na ushawishi wa mara kwa mara wa Roho Mtakatifu Mtakatifu.”1
Hebu fikiria kuhusu hili, kujifunza lugha mpya na kujifunza Lugha ya Roho Mtakatifu vina mengi yanayofanana. Tazama mifanano ifuatayo—inaweza kukusaidia sana kufahamu zaidi kuhusu jinsi ya kupata ufunuo kupitia lugha ya Roho Mtakatifu.
Njia za Kujifunza
Tulipokuwa tukijifunza lugha mpya, kila mtu alikuwa na njia iliyomfaa ili kumuwezesha kukumbuka. Kwangu mimi, kusoma sarufi na kuandika mambo kulinisaidia sana katika kujifunza Kihispania. Wamisionari wengine walipendelea kufanya mazoezi ya kuzungumza na wenza wao. Njia fulani inaweza kumfaa mtu zaidi kuliko nyingine—tafuta inayokufaa zaidi.
Sote hatuhisi wala hatumsikii Roho Mtakatifu kwa njia iliyo sawa. Hebu tuchukulie mfano wa mama yangu. Wakati fulani nilipokuwa nakua, nilipatwa na wasiwasi kuwa nisingeweza kumhisi Roho Mtakatifu kwa sababu sikuwa napata ushawishi kama mama yangu. Kila mara alieleza kuhusu ushawishi uliomjia kama maneno kwenye mawazo yake. Hili halikuwahi kunitokea, hivyo nikachukulia kuwa nisingeweza kuhisi Roho Mtakatifu. Lakini baada ya muda nimegundua kuwa Roho Mtakatifu Mtakatifu mara nyingi huzungumza nami kupitia hisia au mawazo badala ya maneno. Hisia za amani, furaha na upendo ndizo hasa huhusiana na uzoefu wa ufunuo ninaopokea.
Sawa na njia za kujifunza, namna moja ya kumhisi Roho Mtakatifu si bora kuliko nyingine. Kila mmoja wetu ni wa pekee, hivyo Roho Mtakatifu huzungumza nasi kwa njia tofauti. Kwenye kitabu cha Mafundisho na Maagano, tunajifunza kuhusu njia zote ambazo Roho Mtakatifu Mtakatifu hutumia kuzungumza nasi. Anaweza “kutia nuru katika mawazo [yetu],” “kunena amani katika mawazo [yetu],” “kuzungumza [nasi] katika mawazo yetu na katika mioyo [yetu],” au “kuishi katika mioyo [yetu],” au tunaweza kuhisi mwako kifuani mwetu “kuhisi kuwa ni sahihi,” pamoja na njia zingine nyingi (soma Mafundisho na Maagano 6:15, 23; 8:2; 9:8).
Tukiendelea kujifunza maandiko na kufanyia mazoezi kumsikiliza Roho Mtakatifu, tunaweza kugundua jinsi Anavyozungumza nasi.
Omba Usaidizi
Unapojifunza lugha, inaweza kusaidia sana kupata usaidizi kutoka kwa mtu anayefahamu lugha hiyo. Vitabu na nyenzo zingine bila shaka husaidia, lakini kupata usaidizi kutoka kwa mtu anayezungumza lugha hiyo hukuwezesha kujifunza haraka.
Tunapotaka kufahamu zaidi kuhusu Roho Mtakatifu Mtakatifu, tunaweza kupata usaidizi kwa kuwauliza watu tunaowaamini watueleze jinsi wanavyojifunza—wanafamilia, viongozi au marafiki. Lakini muhimu zaidi ni kumuomba Baba wa Mbinguni. Tunaweza kumuomba mambo kama vile fursa zaidi za kumsikia Roho Mtakatifu Mtakatifu au kwa ajili ya msaada wa kutambua wakati tunapopokea ushawishi. Tukinyenyekea, kumwomba Atusaidie, na kuwa na imani kuwa Atatusaidia kufahamu jinisi ya kuhisi Roho Mtakatifu Mtakatifu, Yeye Atatusaidia.
Andika Mambo
Unapojifunza lugha mpya, kuandika mambo unayojifunza kunaweza kukusaidia sana. Nilibeba daftari dogo siku nzima ili kuandika misamiati mipya niliyosikia, kisha ningejaribu kuandika kwenye shajara kwa Kihispania kila usiku ili nifanye mazoezi. Kusahau ni kawaida, hivyo kuandika mambo hutuwezesha kuyarejelea.
Viongozi wetu wametualika kuandika misukumo ya kiRoho Mtakatifu ili tusiisahau.2 Kuandika mambo kama haya kunaweza kutusaidia kuwa na Roho Mtakatifu Mtakatifu katika njia tofauti: (1) Anaweza kutusaidia kukumbuka hisia na misukumo baada ya muda kupita. Huenda ushawishi wa awali ukakusaidia baadaye, au huenda ukakukumbusha kuwa hakika Roho Mtakatifu Mtakatifu amezungumza nawe. (2) Pia ni njia nzuri ya kufuatilia jinsi ulivyohisi Roho Mtakatifu Mtakatifu awali ili uweze kumtambua vyema zaidi ukimhisi baadaye. Hivyo, unaweza kuanza kumtambua Roho Mtakatifu Mtakatifu vyema zaidi.
Endelea kujaribu
Mwisho lakini si ndogo katika umuhimu, usikate tamaa. Hata ikiwa una karama za ndimi, kuna uwezekano mkubwa kuwa hutajifunza lugha mpya kwa siku moja. Kadri unavyoendelea kufanya mazoezi na kutia bidii, utafahamu, lakini unahitaji kuwa na imani na uwe mvumilivu.
Kujifunza kupokea ufunuo na kuwa kwenye mlingano mzuri zaidi na Roho Mtakatifu Mtakatifu ni juhudi ya maisha yote. Nina uhakika kuwa ukiwauliza wazazi wako au viongozi wako wa Kanisa, watasema bado wanaendelea kujifunza. Hivyo usife moyo ukihisi inachukua muda—hauko peke yako! Sote tunahitaji muda kujifunza lugha mpya. Hivyo kuwa na subira, endelea kujaribu, naye Bwana atakusaidia kujifunza lugha ya Roho Mtakatifu Mtakatifu.