2021
Watu huniambia kuwa ni majivuno kusema kwamba sisi ndilo Kanisa pekee la kweli. Je, napaswa kuwaeleza nini?
Januari 2021


“Watu huniambia kuwa ni majivuno kusema kwamba sisi ndilo Kanisa pekee la kweli. Je, napaswa kuwaeleza nini?” Kwa ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Januari 2021, 31.

Kwenye Hoja

Watu huniambia kuwa ni majivuno kusema kwamba sisi ndilo Kanisa pekee la kweli. Je, napaswa kuwaeleza nini?

darasa la kanisa

Bwana Mwenyewe alimwambia Joseph Smith kuwa Kanisa hili ndilo “kanisa pekee la kweli na lililo hai katika uso wa dunia yote, ambalo Mimi, Bwana, napendezwa nalo, nikizungumza na kanisa kwa ujumla na siyo mmoja mmoja” (Mafundisho na Maagano 1:30).

Bila shaka maneno haya hayamaanishi kuwa sisi ni bora kuliko wengine. Lakini yanamaanisha kuwa hili ni Kanisa la Yesu Kristo. Analiongoza, Alilirejesha na Akalipa Mamlaka Yake. Kwa sababu hii, kuna mambo fulani yanayopatikana kwenye Kanisa hili pekee, kama vile manabii na mitume, ibada za hekaluni na maagano, na Kitabu cha Mormoni. Tunashukuru kwa mambo haya, na tungependa kuyashiriki na wengine kwa sababu ya upendo wa kweli—sio kwa sababu tunataka kuwa “sahihi” au “Kanisa lipate waumini zaidi.”

Japo tunaweza kushuhudia kwa ujasiri na bila woga kuhusu Kanisa, kamwe hatupaswi kuwa wenye majivuno kwa wengine au kutoheshimu imani zao. Wakati fulani Nabii Joseph Smith alisema, “Hatusemi watu watupilie mbali mema yao; tunawaomba tu waje wapokee zaidi” (Mafundisho ya Marais wa Kanisa: Joseph Smith [2007], 155).