2021
fMarafiki zangu wote hucheza michezo ya video ya vijana, lakini mimi nimeamua kutocheza. Je, michezo ya video ya vijana INAFAA?
Januari 2021


“Marafiki zangu wote hucheza michezo ya video ya vijana, lakini mimi nimeamua kutocheza. Je, michezo ya video ya vijana INAFAA?” Kwa ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Januari 2021, 30–31.

Maswali na Majibu

“Marafiki zangu wote hucheza michezo ya video ya vijana, lakini mimi nimeamua kutocheza. Je, michezo ya video ya vijana INAFAA?”

Viwango vya Ulimwengu

“Nimeamua pia kutocheza michezo ya video ya vijana. Baadhi yake inafurahisha, lakini hujui kipi kinachoweza kutokea. Mimi hucheza na familia yangu michezo ya kufurahisha, na ninajihisi vyema kutocheza michezo ya video ya vijana. Viwango vya ulimwengu wa leo si sawa na viwango vya Mungu, na ningependa kuwa kama Mungu.”

Payton D., 13, Nevada, Marekani

Msikilize Roho Mtakatifu

“Je, michezo ya video ina lugha au maudhui yasiyofaa? Tunapaswa kuepuka haya, kwa sababu yanamfukuza Roho Mtakatifu. Vurugu pia inaweza kumfukuza Roho Mtakatifu. Kwa makini na kupitia maombi fikiria ikiwa unahisi au hauhisi Roho Mtakatifu maishani mwako unapocheza michezo hii ya video mara kwa mara.”

Miriana B., 18, Washington, Marekani

Mabalozi wa Yesu Kristo

“Ni muhimu kukumbuka kuwa tumejichukulia jina la Yesu Kristo, hivyo sisi ni mabalozi Wake. Katika kila tuyatendayo, tunapaswa kujiuliza ikiwa Angefanya kile tunachokifanya na ikiwa tunasogea karibu Naye zaidi.”

Brandon K., 17, Ohio, Marekani

Nzuri, Bora na Bora Zaidi

“Tunapaswa kukumbuka kuwa kila wakati kuna mambo mazuri, bora na bora zaidi tunayoweza kutazama, kucheza na kusikiliza. Hata ikiwa mambo tunayofanya si ya kuvutia, inawezekana kuwa kuna mambo mengine tunayoweza kufanya pia ambayo ni ya kutia moyo na yenye manufaa.”

Ash H., 17, Virginia, Marekani

Je, Mwokozi Angehisi Vipi?

“Ninapochagua maudhui ya burudani, mimi hujiuliza ikiwa Mwokozi angependezwa kutazama au kucheza mchezo huo pamoja nami. Ikiwa jibu ni hapana, ninaachana na maudhui hayo ya burudani, bila kujali umaarufu wake. Kuna michezo mingi mizuri ambayo ni yenye kuleta changamoto na ya kufurahisha na bado inamwalika Roho Mtakatifu kuwa nasi.”

Brigitte D., California, Marekani

Chapisha