2021
Sikiliza, Tii na Fuata
Januari 2021


“Sikia, Tii na Fuata,” Kwa ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Januari 2021, 32.

NenoMwisho la Mwisho

Sikiliza, Tii na Fuata

Picha
Sikiliza, Tii na Fuata

Neno la kwanza kabisa katika kitabu cha Mafundisho na Maagano ni sikiliza (soma Mafundisho na Maagano 1:1). Linamaanisha “kusikia kwa kusudio la kutii.” Kusikiliza inamaanisha “Kumsikiliza Yeye”— kusikiliza kile Mwokozi anachosema na kisha kufuata ushauri Wake. Katika maneno hayo mawili—“Msikilize Yeye”—Mungu anatupatia mpangilio wa mafanikio, furaha, na shangwe katika maisha haya. Inatubidi kusikiliza maneno ya Bwana, kuyatii hayo, na kufuata kile Alichotuambia!

Je, ni wapi tunaweza kwenda Kumsikiliza Yeye?

Tunaweza kwenda kwenye maandiko. Tunaweza pia Kumsikiliza Yeye hekaluni. Pia tunamsikiliza Yeye vyema zaidi tunapozidi kufahamu jinsi ya kutambua minong’ono ya Roho Mtakatifu. Na, hatimaye, tunamsikiliza Yeye tunapotii maneno ya manabii, waonaji na wafunuzi.

Nini kitatokea kama ukijitoa kwa makusudi kusikiliza, kutii na kufuata kile Mwokozi alichosema na kile Anachokisema sasa kupitia manabii wake? Ninakuahidi kwamba utabarikiwa kwa nguvu ya ziada ya kupambana na majaribu, ugumu, na udhaifu. Ninaahidi miujiza katika mahusiano ya familia yako na kazi zako za kila siku. Na ninaahidi kwamba furaha yako itaongezeka hata misukosuko ikiwa mingi maishani mwako.

Chapisha