2023
Jiunge
Januari 2023


“Jiunge,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Jan. 2023

Jiunge

Tojonirina R.

17, Madagaska

Picha
mvulana

Picha na Valisoa Rakoto

Jina langu ni Tojonirina kutoka Antananarivo, Madagaska. Ninapenda kusikiliza muziki wenye kuburudisha, kusoma vitabu, na kucheza mpira wa kikapu na soka.

Nilipofikisha miaka minane, niliamua kubatizwa. Nilipokuwa ninazamishwa majini, nilijisikia mwenye furaha ambayo ilikuja kutoka kwa Roho. Muda mfupi baada ya ubatizo wangu, mama yangu akafariki. Nilijisikia mwenye huzuni, mwenye mawazo mengi, na mwenye kukanganyikiwa. Hakuna mtoto anayepaswa kujua jinsi unavyojisikia kwa kumpoteza mama yao.

Hata hivyo, miaka mitatu baadae tulikwenda hekaluni na tuliunganishwa kama familia. Hisia ile ya kipekee ya Roho ilinirudia tena siku ile, na nilihisi kwamba mama yangu alikuwepo pembeni yangu hekaluni. Ninayo imani kuwa nitamwona tena siku moja.

Ninajitahidi daima kukumbuka kile nilichokihisi mle hekaluni. Ninamshikilia Roho kwa kujisomea maandiko na kujifunza kuhusu baraka za hekaluni. Wakati jumbe za ulimwengu zinapojaribu kunikanganya, ninajifunza maandiko na kutumaini katika maneno ya manabii. Yananitia moyo na kuimarisha imani yangu.

Chapisha