2023
Kujengwa juu ya Ardhi Imara
Januari 2023


“Kujengwa juu ya Ardhi Imara,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Jan. 2023.

Misingi Imara

Kujengwa juu ya Ardhi Imara

Picha
msichana akiwa na mpira wa maji

Kielelezo na Emily Jones

Nilitazama, nikiwa nimekanganyikiwa, wakati mimi na familia yangu tulipokuwa tukimwagilia zege la msingi wa nyumba yetu. Nilihisi kubezwa. Ni nani ambaye amewahi kusikia nyumba ikimwagiliwa maji? Tulipohamia Texas, Marekani, jirani yetu alieleza kwamba katika eneo hilo tulihitajika kuwagilia maji msingi wa nyumba yetu ili kwamba hali ya hewa isiweze kusababisha nyumba yetu kutitia na kupata ufa. Hivyo nilimwagilia nyumba, ingawaje nilijihisi kuwa mwenye kukanganyikiwa kwa kufanya hivyo.

Umwagiliaji ule ulisaidia kwa muda fulani, lakini hatimaye, nyumba yetu ilianza kupata nyufa. Punde tuligundua kuwa nyumba yetu haikuwa imejengwa juu ya ardhi imara. Ilikuwa imejengwa juu ya dampo, kitu kilichosababisha nyumba yetu kuzama wakati taka zilizokuwa zimefukiwa chini zilipokuwa zikioza kadiri muda ulipokuwa ukipita. Tulimwagilia msingi, lakini bado nyumba yetu iliendelea kupata nyufa. Hivyo hatimaye tulihama.

Tukio hili linanikumbusha umuhimu wa kujenga msingi wangu wa kiroho kwenye ardhi imara ya injili ya Yesu Kristo. Kumekuwa na nyakati ambapo sikuwa nikihisi sadikisho imara la kutosha kuhusu injili. Kwa kuchagua kuamini, “nilimwagilia msingi” wa imani yangu hadi nilipoweza kujenga ushuhuda kwenye ardhi imara ya injili. Nilipochagua kuishi injili ya Yesu Kristo, nilijenga msingi imara ambao hautapata nyufa.

Ann J., Maryland, Marekani

Chapisha