2023
Changamoto ya Chai
Januari 2023


“Changamoto ya Chai,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Jan. 2021.

Misingi Imara

Changamoto ya Chai

Siku moja ya majira ya baridi, nilikuwa nikitembea kwenye viwanja vya shule pamoja na rafiki zangu Alice na Trevor wakati tulipofikia alama iliyosomeka: “Vikombe vya chai sasa vinapatikana.” Kwa shauku, Trevor alijitolea kutununulia kila mmoja wetu kikombe cha chai. “Hapana, asante,” mimi nilijibu.

Trevor alijitolea kuninunulia chai kila siku, nami niliendelea kukataa. Mwishowe, aliniuliza kwa nini mimi sinywi chai. Nilimwambia juu ya Neno la Hekima, nikitumaini kwamba angeelewa. Lakini yeye aliligeuza kuwa mzaha mkubwa. Alijaribu kunifanya mimi nivunje Neno la Hekima.

“Siyo kama unakunywa dawa za kulevya,” alisema. “Kikombe cha chai hakina madhara!”

Wiki iliyofuatia, yeye na rafiki zake walianza kunikejeli vibaya zaidi. Nilijaribu kupuuzia, ingawa haikuwa rahisi.

Baada ya muda, walianza kujisikia vibaya kutokana na matendo yao na wakaacha kunikejeli. Siku moja, mwalimu wangu aliniambia: “Wewe daima umekuwa mfano wa imani na dini yako. Ninaona fahari juu yako.”

Ninajionea fahari pia. Daima si rahisi, lakini najua kuwa nitabarikiwa kwa kusimamia viwango vyangu.

Nicolé M., West Midlands, Uingereza

Chapisha