“Imani katika Giza,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Desemba 2022.
Imani katika Giza
Hapa kuna mapendekezo machache ambayo yamenisaidia mimi nikiwa na maswali na mashaka.
Nilipokuwa kijana mdogo, familia yangu mara kwa mara ilikuwa ikitembelea Hifadhi ya Taifa ya Great Basin huko Nevada, Marekani. Kitu cha kipekee katika hifadhi hii ni Mapango ya Lehman.
Mwongozaji wa watalii anakuongoza hadi ndani ya pango na, katika hatua fulani, anazima taa zote. Hapo unaona giza totoro. Ni hisia nzito, na wazo la kuipata njia ya kutoka nje ya pango pasipo taa linatisha. Kwa shukrani, mwongozaji daima huwasha taa tena na kukuongoza kutoka nje kwa usalama.
Nyakati zingine tunakabiliwa na maswali na hata mashaka kuhusu Kanisa na shuhuda zetu. Yanaweza kuwa mazito na yasiyo na uhakika, kama vile kuwa ndani ya pango lenye giza.
Ni kawaida kuwa na maswali na wasiwasi. Kitu kitakacholeta tofauti kubwa ni jinsi unavyoyakabili.
Hapa kuna mapendekezo machache ambayo yamenisaidia mimi.
Onyesha Imani
Nimekuja kujua kwamba kama ninayakabili maswali na mashaka kutoka kwenye msimamo wa imani, daima ninaweza kuipata njia ya kusonga mbele. “Imani siyo kuwa na ufahamu kamili wa vitu” (Alma 32:21). Na “ikiwa hamwezi ila kutamani kuamini, acha hamu hii ifanye kazi ndani yenu” (Alma 32:27).
Ulimwengu utakuambia kwamba kama huwezi kuthibitisha kitu kwa kiwango cha kisayansi, hakiwezi kuwa kweli. Hii sio njia ya Bwana. Kama vile Mwokozi alivyomwambia Tomaso, ambaye asingeweza kuamini bila kugusa majeraha ya vidonda vya Mwokozi yeye mwenyewe, “Wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye” (Yohana 20:27).
Omba, Tafuta, Bisha
Kifungu cha maneno “omba, tafuta, bisha” kinarudiwa rudiwa katika maandiko (ona Mathayo 7:7; Mafundisho na Maagano 88:63). Njia ya Bwana ya kutusaidia sisi kwa maswali yetu ni kwa sisi kumwuliza Yeye Maswali.
“Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu” (Yakobo 1:5). Nenda moja kwa moja kwenye chanzo cha ukweli wote. Mungu anakupenda na atakusaidia.
Kuwa Mtafutaji wa Ukweli
Nimegundua kwamba kwa wale walio waaminifu na kwa unyenyekevu wanatafuta ukweli, hatimaye mara nyingi watapata majibu ya maswali yao. Kwa upande mwingine, kwa wale ambao wanatafuta ili kupata makosa wataenda mbali na mbali zaidi kutoka kwenye ukweli.
Kuwa mtafutaji wa ukweli. Ukweli upo, na unaweza kuupata.
Tengeza Saduku la “Litajibiwa Baadaye”
Hivyo basi unafanya nini kama kwa unyenyekevu na kwa dhati kabisa unatafuta majibu na hayaonekani kuja?
Tena, nachagua kuyakabili kwa imani. Nimejitengenezea kijisanduku katika rafu za akili yangu—kama kisanduku kidogo kizuri cha hazina. Kilichoandikwa juu yake ni maneno “Litajibiwa Tarehe za Baadaye.”
Wakati wowote niwapo na swali au mashaka ambayo siwezi kutatua, ninayaandika kwenye karatasi ya kufikirika, naikunja vizuri na kuiweka katika kisanduku hicho. Kisha nakirudisha juu ya rafu.
Kwa kufanya hivyo, ninatenda kwa imani kwamba siku moja Bwana atajibu swali hilo. Labda atajibu, pengine hatajibu. Hilo ni juu yake Yeye na katika hekima Yake.
Licha ya hayo, baadhi ya maswali yangu yamejibiwa. Lakini mengi bado yapo ndani ya kisanduku. Na mimi NAKUBALIANA na hilo.
Rafiki zangu wapendwa katika Kristo, iweni watafutaji wa ukweli.
Imani yako inapoongezeka, Bwana atakuwa pamoja na wewe. Na unapomwendea Yeye kwa imani, Yeye atakufunulia mambo unayohitaji kuyajua kwa wakati sahihi.