2023
Mto Yordani
Januari 2023


“Mto Yordani,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Jan. 2023.

Maeneo kutoka kwenye Maandiko

Mto Yordani

Je, ni nini kilifanyika hapa na kitu tunachoweza kujifunza kutokana na hicho?

Uko wapi?

Picha
Mto Yordani

Ramani kutoka Getty Images

Chanzo chake kiko kwenye Mlima Hermoni upande wa Kaskazini.

Unatitirika kuelekea Kusini kwenye Bahari ya Galilaya—na unatoka tena.

Unaishia kwa kutiririkia kwenye Bahari ya Mauti.

Kwa sehemu kubwa ya urefu wake, uko chini ya usawa wa bahari.

Ni mto ulio muhimu sana katika eneo hili.

Je, Ni nini Kilitokea Hapa?

Yoshua aliwaongoza wana wa Israeli kuvuka Mto Yordani kwenye nchi kavu ili kuingia katika nchi ya ahadi (ona Yoshua 3–4).

Picha
Yohana Mbatizaji anambatiza Yesu Kristo

Yesu Kristo alibatizwa katika Mto Yordani na Yohana Mbatizaji (ona Mathayo 3).

Chapisha