2023
Mahali Pangu Ninapopapenda pa Kutafakari
Januari 2023


“Mahali Pangu Ninapopapenda … pa Kutafakari” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Jan. 2023.

Mahali Pangu …

Ninapopapenda pa Kutafakari

Je, una mahali unapopenda pa kutafakari?

Wakati unapotafakari, unapata mtazamo zaidi wa kiroho. Inaweza pia kukusaidia wewe kuboresha afya yako ya akili kwa kusafisha kichwa chako kutokana na mkanganyiko na msongo wa mawazo ambao huja kutokana na majaribu na mahangaiko ya maisha ya siku hadi siku. Baadhi ya watu hata huwa na mahali maalum ambapo wao hupapenda pa kutafakari. Ona baadhi ya sehemu hizi za kutafakari zilizoelezwa na vijana wengine!

Tafakari: Kutafakari kunamaanisha kufungua akili na moyo kwa ajili ya misukumo ya Roho Mtakatifu unapokuwa unajifunza na kufikiria kuhusu injili. Tafakuri ya kweli, ambayo inaweza kufanyika mahali popote, inahitaji kwamba ufanye kazi fulani ya kiroho unapokuwa unatafuta ufunuo.

Nje ya Maji

msichana

Mahali pangu ninapopapenda pa kutafakari ni kwenye eneo lolote lenye maji, kama vile ziwa au bahari. Katika picha hii nilikuwa kwenye boti ya babu yangu. Ninapenda kuwa hapo kwa sababu ninahisi kuwa karibu zaidi na Roho, hususani wakati wa mawio au machweo. Ninapata kupokea mwongozo wa kiungu na kuja na mawazo yangu yote yaliyo bora hapo.

Macey M., 16, Texas, Marekani

Pata Muda wa Kuwa Peke Yako

mvulana

Mahali pangu bora zaidi pa kutafakari ni wakati nikiwa peke yangu. Natafakari wakati wote, niwapo bafuni au mahali penye ukimya kama vile nyumbani wakati wa kujifunza kwangu maandiko. Ninakwenda kuendesha baiskeli na nyakati zingine ninasikiliza Njoo, Unifuate kwenye podikasti. Ninajipa muda wa kuwa peke yangu kukaa kwenye mazingira mazuri ya asili na kutafakari hapo vile vile.

Grant R., 14, Texas, Marekani