2023
Je! Mamajusi walikuwa akina nani?
Januari 2023


“Je! Mamajusi walikuwa akina nani?,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Jan. 2023.

Kwenye Hoja

Je! Mamajusi walikuwa akina nani?

mmoja wa Mamajusi

Maandiko yanatuambia kwamba “mamajusi [walikuja] kutoka mashariki” (Mathayo 2:1) kumtafuta Mwokozi. Hili neno mamajusi linatokana na neno la Kiajemi, magi. Ingawa hatuambiwi watu hawa walikuwa akina nani hasa, kuna mambo machache tunayoweza kusema tunayajua kuhusu watu hawa kutokana na kile ambacho tunaambiwa.

Watu kwa mazoea tu wanafikiri kwamba kulikuwa na Mamajusi watatu kwa sababu walileta zawadi tatu. Lakini haiko wazi kwenye maandiko ni Mamajusi wangapi hasa walikuwepo. Pia tunaelewa kwamba walimtembelea Yesu akiwa mtoto mdogo na siyo mtoto mchanga (ona Mathayo 2:11).

Ni wazi kabisa Mamajusi walikuwa watu waadilifu na walijua baadhi ya unabii kuhusu kuzaliwa kwa Masiya. Yawezekana walitoka kwenye tawi la watu wa Bwana. Kwa bidii walimtafuta Mwana wa Mungu na waliongozwa Kwake na Roho. Walimletea zawadi na kisha wakarejea kwao ili watoe ushahidi kwa watu wao. Pia walionywa katika ndoto wasimwambie Herode mahali alipo mtoto.

Uaminifu wao na bidii yao vinaweza kuwa mfano wa kuvutia kwetu sisi katika safari zetu binafsi za kusogea karibu zaidi na Mwokozi.