2023
Kupata Furaha katika Huduma ya Muziki
Januari 2023


“Kupata Furaha katika Huduma ya Muziki,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Jan. 2021.

Misingi Imara

Kupata Furaha katika Huduma ya Muziki

Picha
mvulana akipiga kinanda

Kielelezo na Emily Jones

Nilianza masomo ya kujifunza kupiga kinanda nikiwa na umri wa miaka saba. Mwanzoni, ilikuwa vigumu kusoma noti za muziki na kuwa makini wakati wa masomo yangu. Sikuwa tu nikipenda kufanya mazoezi ya kinanda.

Baadaye mama yangu aliniambia nipige kinanda wimbo “When I Am Baptized” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 103) wakati wa ubatizo wangu. Ilikuwa mara ya kwanza kwangu kupiga kinanda Kanisani. Nilikuwa mwenye hofu lakini nilihisi kuridhika nilipofanya hivyo.

Muda mfupi baadaye nikawa mwenye shughuli nyingi za shule na nikataka kuacha kupiga kinanda, lakini wazazi wangu walinitia moyo niendelea kujifunza. Walisema ikiwa ningeendelea kupiga, ningeweza kupata shangwe katika kumtumikia Bwana.

Kutokea hapo, nilipenda kupiga kinanda. Nilianza kupiga kinanda katika mkutano wa sakramenti na wakati nilipofikia umri wa miaka 12, niliitwa rasmi kuwa mpiga kinanda wa kata. Nilikuwa na furaha sana! Nilipiga kinanda wakati wa mawasilisho ya Msingi na niliongozana na kwaya ya kata yetu wakati wa mikutano ya kata na ibada nyinginezo. Niliitwa hata kuwa mpiga kinanda wa kigingi na nilipiga wakati wa mkutano wa kigingi.

Ninawashukuru wazazi wangu kwa kunitia moyo nijitahidi kufanya kwa uwezo wangu wote. Daima nitakuwa mwenye shukrani kwa Baba wa Mbinguni kwa kipaji ambacho Yeye amenipatia. Ninajua nitaweza kutumia vipaji vyangu kwenye misheni yangu na katika huduma nyinginezo siku zijazo. Kweli ninapata shangwe katika kumtumikia Bwana.

Jyle S., National Capital Region, Ufilipino

Chapisha