2023
Zaidi Kama Kristo
Januari 2023


“Zaidi Kama Kristo,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Jan. 2023.

Zaidi Kama Kristo

Yesu Kristo

Sehemu mojawapo ya programu ya Watoto na Vijana ni kujitahidi kuwa zaidi kama Kristo kwa kukua kiroho, kijamii, kimwili, na kiakili (ona Luka 2:52). Amini usiamini, kufanyia kazi malengo hakupaswi kuwa vigumu kama vile wewe unavyofikiri. Angalia jinsi vijana ulimwenguni kote wanavyokua na kuwa zaidi kama Kristo!

Kiroho

msichana

Jina: Catalina

Mahali: Chile

Lengo: Kusoma maandiko na kusali kila siku

“Ninajaribu kuwa karibu na Roho kwa kusali. Ninasali kila usiku kabla ya kwenda kitandani kulala na kisha ninasoma maandiko. Ninafanya kazi kwa bidii ili kuyaelewa vyema zaidi. Ninaposoma na kusali kila siku, ninahisi amani na kuwa karibu zaidi na Mungu.”

Kijamii

msichana

Jina: Raisa

Mahali: Samoa

Lengo: Kuwajua wasichana wa darasani kwake vizuri zaidi

“Yawezekana nikajua jina la kila msichana katika kata yangu, lakini sikuwa nawajua wao ni akina nani au walipenda nini. Hivyo nilianza mmoja baada ya mwingine kwa kila msichana na kwa mtu asiyependa kujumuika kama mimi, nilifurahia jinsi nilivyogundua mambo mengi tuliyonayo yanayofanana. Kadiri nilivyotumia muda ili kuwafahamu, ndivyo nilivyowaona mabinti hawa warembo katika njia ambayo Baba wa Mbinguni anawaona.”

Kimwili

mvulana

Jina: Eugene

Mahali: Kenya

Lengo: Kuwa bora kwenye mpira wa miguu (soka)

“Nilianza kufanya mazoezi na timu ya marafiki mwezi uliopita. Mazoezi yamenisaidia kuelewa kwamba Mungu hataki sisi tufanye hili peke yetu. Tunaweza kuungana na rafiki zetu katika malengo yetu ya kuwa kama Mwokozi. Anajua kwamba sisi tunahitajiana ili tufanikiwe. Kama tunasali, Yeye ataweka watu katika maisha yetu ili watusaidie kuwa katika ubora wetu.”

Kiakili

mvulana

Jina: Jackson

Mahali: South Carolina, Marekani

Lengo: La muda-mrefu: Kumiliki lori la chakula siku moja; la muda-mfupi: Kujifunza kutengeneza chakula

“Nilimwambia mmoja wa viongozi wangu wa Vijana kuhusu lengo nililonalo la kuwa na lori la chakula. Yeye alisema, ‘Kila mwaka mimi ninafanya sherehe ya kurejea shuleni. Kwa nini usije kutupikia?” Nilifanya hivyo. Nilitengeneza takriban soseji 50 pamoja na baga ndani ya dakika 45. Nilipenda kuwa pamoja na vijana wenzangu kutoka katika akidi yangu, na nilipata mrejesho na sifa nzuri sana kutokana na tukio hili. Na nilijifunza mengi.”