Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Fikia Nguvu Zake
Machi 2024


“Fikia Nguvu Zake,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Machi 2024.

Kuhusu Toleo Hili Maalumu

Fikia Nguvu Zake

Katika Injili ya Marko, tunasoma kuhusu mwanamke aliyekuwa mgonjwa kwa miaka 12. Mtu fulani alimwambia kuhusu Yesu. Basi, alipoingia katika mji wake, aliketi kando ya njia, akingojea. Alipokuwa akipita, alinyosha mkono kimya kimya ili kugusa pindo la vazi Lake.

Aliponywa mara moja. Lakini si yeye pekee aliyeona muujiza huo; Yesu pia aligundua. “Mara Yesu, hali akijua nafsini mwake ya kuwa nguvu zimemtoka, akageuka kati ya mkutano, akasema, Ni nani aliyegusa mavazi yangu?” (Marko 5:30). Wema pia unaweza kumaanisha nguvu. Yesu alijua mara moja mtu fulani alikuwa amepokea nguvu kutoka Kwake. Mwitikio wake wa papo hapo ulikuwa ni kumpata, kuzungumza naye na kumkumbusha juu ya nguvu ya imani. Alimwita “binti.” Kupitia Yeye, alifanywa mzima.

Nimejifunza kwamba sala ya kuomba nguvu huwa haiachwi bila kujibiwa. Ikiwa tunamfikia, Yeye “hufikia hatua yetu” (ona Nyimbo za Dini, na 62) Kila makala katika gazeti la mwezi huu ni ukumbusho wa ukweli huo.

Katika Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi, Urais wa Kwanza unafundisha kwamba “Mwokozi … ni ‘nguvu ya vijana’” ([2022], 2). Labda unajiuliza jinsi gani ya kupata nguvu hizo. Ni matumaini yangu kuwa utapata kitu ndani ya kurasa hizi ambacho kitakuongoza kumfikia.

Pekua kurasa hizi. Tafuta maneno ya matumaini, tafuta andiko lenye nguvu, andika misukumo ambayo imeacha hisia kwenye moyo wako. Kupitia Yesu Kristo, wewe pia utafanywa kuwa mzima.

Emily Belle Freeman

Kwa upendo mkubwa,

Emily Belle Freeman

Rais Mkuu wa Wasichana