Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Ni Lini Nitaacha Kuhisi Hatia na Aibu?
Machi 2024


“Ni lini nitaacha Kuhisi Hatia na Aibu?,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Machi 2024.

Nguvu ya Kuishinda Dhambi

Ni Lini Nitaacha Kuhisi Hatia na Aibu?

Wakati mwingine inaweza kuonekana kuwa rahisi kuhisi kutokuwa na tumaini kuhusu wewe mwenyewe kuliko kuhisi upendo ambao Mwokozi anao kwako—lakini kama Nefi alivyojua, si lazima iwe hivyo.

Picha
Nefi akiandika kwenye mabamba

Unapofanya kitu kibaya, unaweza kuwa na mawazo juu ya akili yako kwamba wewe umeshindwa. Kwamba ulipaswa kujua zaidi. Kwamba hufai kupendwa.

Moyoni mwako, wewe unajua kwamba hakuna kati ya mambo hayo ni ya kweli. Umejifunza kuhusu thamani yako kama mwana au binti wa Mungu, na unajua kwamba toba ni ya kweli na inawezekana. Lakini bado, baada ya kufanya dhambi au kufanya kosa, unaweza kujaribiwa kujiadhibu zaidi kuliko mtu mwingine yeyote kwa mawazo ya hatia na aibu.

Hata baadhi ya wahusika wetu tuwapendao wa maandiko walihisi hivi nyakati fulani.

Hata Nefi?

Baada ya kuandika kuhusu kifo cha baba yake, Nefi aliandika “Walakini, ingawa Bwana ana wema mkubwa, hata kunionyesha kazi yake kuu na ya maajabu, moyo wangu unalia: Ewe mimi mtu mwovu! Ndiyo, moyo wangu unahuzunishwa kwa sababu ya mwili wangu; moyo wangu unahofishwa na dhambi zangu. Nimezingirwa, kwa sababu ya majaribio na dhambi ambazo zinaninasa kwa urahisi. Na ninapotaka kushangilia, moyo wangu huugua kwa sababu ya dhambi zangu” (2 Nefi 4:17–19).

Huyu ndiye Nefi tunayemzungumzia—mtu yule yule ambaye aliokoa mabamba ya shaba kutoka kwa Labani, akatengeneza upinde kutoka nyikani na akajenga merikebu bila kuwahi kujenga moja hapo awali. Alikuwa na ushuhuda wa wema wa Bwana; hata hivyo, alijiona hafai kwa sababu ya dhambi na udhaifu wake.

Tunapaswa tufanye nini? Ikiwa shujaa wetu wa Kitabu cha Mormoni alipambana na hisia za hatia na kutotosheleza, tunaweza kufanya nini tunapohisi vivyo hivyo?

Cha Msingi Ni Fokasi juu ya Yesu Kristo

Hadithi ya Nefi haikuishia hapo. Lengo kuu la Nefi lilikuwa ni kuhamisha umakini wake kutoka kwake hadi kwa Yesu Kristo.

Nefi anapoomboleza, anasema, “Walakini, ninajua ninayemwamini. Mungu wangu amekuwa tegemeo langu” (2 Nefi 4:19–20).

Baada ya mabadiliko haya ya mawazo, shujaa wetu wa maandiko haangazii tena uchungu anaohisi kutokana na makosa yake. Badala yake, anafurahi katika Mwokozi wake! Nefi anasema, “Shangilia, Ewe moyo wangu, na umlilie Bwana, na kusema: Ewe Bwana, nitakusifu milele; ndiyo, nafsi yangu itashangilia ndani yako, Mungu wangu, na mwamba wa wokovu wangu” (2 Nefi 4:30).

Kama vile Nefi, unaweza kupata rehema, msamaha na amani kupitia Yesu Kristo. Unaweza usihisi kama unaweza kujipa neema, lakini kuna Mmoja ambaye atafanya. Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alisema, “Neema ya Kristo hutupatia sio tu wokovu kutokana na huzuni na dhambi na mauti lakini pia wokovu kutokana na ukaidi wetu wa kujikosoa.”1

Kwa hivyo unapohisi kupotea sana kwamba huoni njia ya kushinda dhambi na makosa yako, ujue kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo hawajaacha kukupenda. Weka mtazamo wako kwa Mwokozi wako, na anaweza kukusaidia kushinda dhambi zako na hatia yako.

Chapisha