Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Wakati Huzuni Ijapo
Machi 2024


“Wakati Huzuni Ijapo,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Machi 2024.

Nguvu Katika Nyakati za Huzuni

Wakati Huzuni Ijapo

Maisha yanapokushusha chini, Yesu Kristo anaweza kukuinua kwa tumaini.

kijana akionekana na huzuni, na mawingu meusi juu yake

Vielelezo na Dean MacAdam

Unaweza kufika mbali sana maishani kupitia juhudi na bidii. Unaweza kwenda kulala mapema, kuamka mapema (ona Mafundisho na Maagano 88:124), na ujaze kila siku tabia za haki na nidhamu binafsi.

Lakini bado, siku zingine zitakuwa ngumu zaidi kuliko zingine.

Na kisha siku zingine … ndio, zinaonekana ngumu sana kwamba unaweza kuanza kufikiria kuwa siku nzuri zimepita milele.

Unafanya nini kwenye siku hizo? Unafanya nini wakati juhudi zako bora, ikijumuisha juhudi zako bora za kuishi maisha ya haki (maombi, kufunga, kusoma maandiko, kuhudhuria kanisani na hekaluni, nk.), hazionekani kutosha? Unapojaribu na kujaribu dhidi ya kukata tamaa, lakini inaonekana kurudishwa nyuma kwa kasi zaidi?

Unamgeukia Yesu Kristo, bila shaka. Tumaini ni karama ya Kiroho (ona Moroni 8:26). Na karama zote za kiroho hutoka kwa Yesu Kristo (ona Moroni 10:17).

Wakati magumu ya maisha yanaposhuka juu yako kama mlima unaoanguka kutoka angani, zawadi ya kiroho ya tumaini inaweza kuwa yako unapofokasi zaidi kwa Yesu Kristo.

“Bwana Hupunguza Mizigo Yangu”

Maisha tayari yalikuwa magumu kwa watu wengi wa Venezuela kabla ya janga la UVIKO-19 mnamo 2020, lakini kwa wakati huo hata mahitaji ya msingi yalikuwa magumu. Kwa Sebastian mwenye umri wa miaka 11 na familia yake, nguvu kutoka kwa Yesu Kristo zilihitajika ili kuendelea kuwa mchangamfu na mwenye furaha nyakati za huzuni. “Ninahisi vibaya wakati hatuwezi kununua bidhaa muhimu kama vile chakula, nguo na dawa,” Sebastian anasema. “Lakini nina imani Bwana ataendelea kutubariki. Ninahisi kubarikiwa kwamba niliweza kupokea baraka zangu za patriaki. Inaniambia kuhusu mambo niliyoahidiwa kabla sijaja duniani.”

Kufokasi kwa Yesu Kristo kama sehemu ya mada ya vijana ya mwaka jana (“Nayaweza mambo yote katika Kristo” [Wafilipi 4:13]) kumethibitika kuwa msaada mkubwa. “Kwa sababu ya matatizo yanayoikabili nchi yangu, mada ya vijana kutoka mwaka jana ilinikumbusha kwamba Kristo atanisaidia kushinda na kufanya mambo yote kupitia Yeye,” Sebastian anasema.

Imekuwa safari ndefu, lakini Sebastian na familia yake wameona baraka na matumaini njiani. “Bwana hunipunguzia uzito wa mizigo Yangu”, asema. “Ninapohuzunika, mimi huomba, kusoma maandiko na kusoma baraka zangu za patriaki. Shukrani Kwake, biashara yetu ya familia ya shuleni na ofisini ambayo tuliianza miaka mitatu iliyopita imekuwa na mafanikio zaidi mwaka huu. Ningependa kuwaambia vijana wengine kwamba wanapaswa kuwa tayari daima kumtegemea Yesu Kristo. Ninapofanya hivyo, ninaweza kushinda changamoto zangu.”

Nguvu kupitia Fokasi Nzuri

Nabii Nefi, ambaye alivumilia mateso magumu maishani mwake, alifundisha ukweli huu mzuri:

“Msonge mbele mkiwa na imani imara katika Kristo, mkiwa na mg’aro mkamilifu wa tumaini, na upendo kwa Mungu na wanadamu wote. Kwa hiyo, kama mtasonga mbele, mkila na kusherehekea neno la Kristo na mvumilie hadi mwisho, tazama, hivi ndivyo asema Baba: Mtapokea uzima wa milele” (2 Nefi 31:20).

Tumaini, chanzo chenye nguvu cha nguvu dhidi ya huzuni, huja tunapofokasi kwa Yesu Kristo. Je, ni wakati wa kuelekeza umakini wako Kwake zaidi kidogo?