Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Fikia Nguvu Zake—Sasa na Daima
Machi 2024


“Fikia Nguvu Zake—Sasa na Daima,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Machi 2024.

Nguvu Wakati Wote

Fikia Nguvu Zake—Sasa na Daima

Unastahili nguvu na usaidizi wa Yesu Kristo.

Picha
kijana kwenye kichaka cha miiba

Vielelezo na Alex Nabaum

Hebu wazia ukitembea msituni na kukutana na mvulana mdogo aliyejikwaa na kuangukia kwenye matawi yaliyokufa. Moja yatawi ni zito sana kwake kulinyanyua peke yake.

Je, unasaidia? Au unaketi kwanza na kuamua ikiwa hata anastahili usaidizi wako?

Bila shaka unasaidia! Wazo la kuzuia usaidizi wako hadi mvulana awe mwenye kustahili linaweza kuonekana kuwa la kipuuzi kwako. Na bado tunafikiri hivi kuhusu sisi wenyewe—isipokuwa, katika hali hii, sisi ni mtoto mwenye uhitaji huo.

Unastahili Kuokolewa

Bila kujali umri wako, wewe ni mtoto ukilinganishwa na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. (Kwa kweli, wewe ni mtoto halisi wa Baba wa Mbinguni.) Na nguvu zako—za kimwili, kihisia, kiroho, au za kiakili—si kitu ikilinganishwa na Zao. Wengi wetu tunaelewa dhana hiyo vya kutosha. Lakini tunapojikwaa kwa sababu yoyote ile, mara nyingi sana tunahisi kwamba hatuwezi kufikia usaidizi hadi tuupate. Hiyo siyo kweli kabisa.

Rais Dieter F. Uchtdorf, wakati huo—Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza, aliwahi kuzungumza kuhusu mfano wa kondoo aliyepotea katika Luka 15.

“Je, kondoo wanahitaji kujua jinsi ya kutumia mashine ya kujua mahali?” aliuliza. Je, wanahitaji kujua kutumia GPS kujua mahali alipo? Je, wanahitaji kuwa na utaalamu wa kujenga programu ambayo itaomba msaada? Je, kondoo wanahitaji idhinisho la mdhamini kabla ya Mchungaji Mwema kuja kumwokoa?

“Hapana. Hakika sivyo! Kondoo anastahili kuokolewa kwa sababu anapendwa na Mchungaji Mwema.

“Kwangu mimi, mfano wa kondoo aliyepotea ni mojawapo ya vifungu vya matumaini katika maandiko yote.”1

Kila mmoja wetu anaweza kupotea kwa sababu nyingi tofauti. Na kwa kila mmoja wetu, msaada wa kiungu unaweza kuwa tayari unatutafuta.

Picha
mkono wa Bwana ukiufikia mkono wa kijana katika kichaka cha miiba

Msaada Unapatikana Daima

Usaidizi unapatikana kwetu sio tu tunapotenda dhambi, lakini pia tunapoishi maisha bora tuwezavyo. Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha:

“Nashangaa kama tunashindwa kukiri kikamilifu kipengele hiki cha kuimarisha cha Upatanisho maishani mwetu na kuamini kimakosa kwamba lazima tubebe mzigo wetu peke yetu—kupitia unyonge, nguvu, na nidhamu na kwa uwezo wetu ulio na mipaka.

“Ni jambo moja kujua kwamba Yesu Kristo alikuja duniani kufa kwa ajili yetu. Lakini pia tunahitaji kufahamu kwamba Bwana anatamani, kupitia Upatanisho Wake na kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, kutuhuisha sisi—sio tu kutuongoza bali pia kutuimarisha na kutuponya.”2

Unastahili msaada Wake! Bila kujali njia uliyopitia hivi majuzi, Yesu Kristo anasimama tayari kutembea nawe sehemu inayofuata.

Picha
kijana na Yesu Kristo wakitembea mbali na matawi yenye miiba

Chapisha