Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Ngumu Kuliko Majaribu
Machi 2024


“Ngumu Kuliko Majaribu,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Machi 2024.

Nguvu ya Kuishinda Dhambi

Ngumu Kuliko Majaribu

Mwokozi anaweza kukuimarisha unapotafuta kuepuka dhambi.

Toba ni muujiza. Yesu Kristo alifanya hili liwezekane. Baba wa Mbinguni anafurahi kutusamehe tunapochagua kutubu na kufuata amri Zake. Ingawa sisi sote tutahitaji kutubu katika maisha yetu yote, tunawezaje kupinga dhambi na kufanya maamuzi bora?

Hapa kuna vidokezo vya kupata nguvu kupitia Yesu Kristo dhidi ya Majaribu.

  • Soma maandiko kila siku.

  • Sali kila siku.

  • Nendeni kanisani mara kwa mara.

Wakati mwingine tunatupilia mbali haya kama majibu ya kawaida na dhahiri. Usiingie katika mtego huo! Majibu haya ya msingi na ya muhimu yanarudiwa mara kwa mara kwa sababu ndiyo majibu ya msingi! Yanafanya kazi.

Fanya mambo haya, na utamkaribia zaidi Mwokozi wako.