“Njia 7 za Kufikia Nguvu za Yesu Kristo,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana , Machi 2024.
“Yesu Kristo ni nguvu kwa vijana.” Hili ni zaidi ya wazo kuu. Ni ukweli wenye nguvu uliofundishwa na manabii na mitume1 —lakini ikiwa tu tutautumia, ikiwa tunamfanya Yesu Kristo kuwa chanzo cha nguvu zetu. Lakini ni kwa jinsi gani tunaweza kufanya hivyo? Je, tunamruhusuje Yesu Kristo atusaidie kuwa na nguvu zaidi? Hapa kuna mawazo machache.
Vielelezo na Toby Newsome
1 Pokea Nguvu kwa Kushika Maagano Yako
“Ni kipi chanzo cha nguvu [zetu] za kimaadili na kiroho na tunakipataje? Chanzo ni Mungu. Njia yetu ya kufikia nguvu hiyo ni kwa njia ya maagano yetu na Yeye.”
Mzee D. Todd Christofferson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, Aprili 2009 mkutano mkuu (Ensign au Liahona, , Mei 2009, 20).
2 Pokea Nguvu kwa Kusoma Neno Lake
“Neno la Mungu … lina nguvu za kuimarisha Watakatifu … ili waweze kushinda uovu, kushikilia kwa nguvu wema, na kupata shangwe katika maisha haya”
Rais Ezra Taft Benson (1899–1994), “Nguvu ya Neno,” mkutano mkuu wa Apr. 1986 (Ensign , Mei 1986, 80).
Maandiko yanaweza kutuliza roho iliyofadhaika, kutoa amani, tumaini na urejesho wa kujiamini katika uwezo wa mtu wa kushinda changamoto za maisha. Yana uwezo wenye nguvu ya kuponya changamoto za kihisia kama imani katika Mwokozi ikiwepo.”
3 Pokea Nguvu kwa Kushika Amri Zake
“Usalama wetu upo katika toba. Nguvu zetu huja kwa utiifu kwa amri za Mungu.”
Rais Gordon B. Hinckley (1910–2008), “The Times in Which We Live ,” mkutano mkuu wa Okt. 2001 (Ensign , Nov. 2001, 74).
“Kama ikiwa kwamba watoto wa watu watatii amri za Mungu atawalisha, na kuwatia nguvu.”
4 Pokea Nguvu kwa Kutubu Kila Siku
“Kupitia imani katika Upatanisho wa Yesu Kristo na toba ya dhambi zao, [watu binafsi] hupokea nguvu na msaada wa kufanya kazi nzuri ambayo vinginevyo hawangeweza kuifanya kama wakiachwa kwa njia zao wenyewe.
Kamusi ya Biblia, “Neema ,” Gospel Library.
5 Pokea Nguvu kwa Kutafuta na Kufuata Ufunuo
Nini kitatokea kama ukiamua kwa makusudi kusikiliza, kutii na kufuata kile Mwokozi alichosema na kile anachokisema sasa kupitia manabii wake? Ninakuahidi kwamba utabarikiwa kwa nguvu ya ziada ya kupambana na majaribu, ugumu na udhaifu. … Na ninaahidi kwamba furaha yako itaongezeka hata misukosuko ikiwa mingi maishani mwako.”
Russell M. Nelson, “Msikilize Yeye ,” mkutano mkuu wa Aprili 2020 (Ensign au Liahona , Mei 2020, 90).
“Mstari wetu wa nguvu za kiroho unaimarishwa kupitia sala. Tunaposhauriana na Mungu katika matendo yetu yote, atatuongoza kwa wema.”
Rais Russell M. Nelson, mkutano mkuu wa Okt. 1984 (Ensign , au Liahona, Nov. 1984, 31).
7 Pokea Nguvu kupitia Huduma ya Hekalu
“Tafadhali tengeni muda kwa ajili ya Bwana katika nyumba Yake takatifu. Hakuna kitakachoimarisha msingi wako wa kiroho kama huduma ya hekaluni na kuabudu hekaluni.