Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Kushughulikia Udhaifu Ndio Kazi Maalumu ya Mwokozi
Machi 2024


“Kushughulikia Udhaifu Ndio Kazi Maalumu ya Mwokozi,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Machi 2024.

Nguvu katika Udhaifu

Kushughulikia Udhaifu Ndio Kazi Maalumu ya Mwokozi

Yesu Kristo anaweza kutusaidia kukua wakati tu matatizoni, na si tu kuyapitia.

Picha
mvulana akionekana mdhaifu

Vielelezo na Uran Duo

Mason hahisi upendo wa Mungu kama zamani. Amekuwa akipambana na tiba ya msongo wa mawazo kwa miaka michache kwa mafanikio kidogo, na ana wasiwasi kwamba ndoto zake haziwezi kutimizwa.

Anna anasikia vijana wengine wakizungumza kuhusu uzoefu wenye ufunuo na miujiza. Ingawa anajaribu, hahisi kama anapata majibu au kuwa na uzoefu wa kiroho kama kila mtu mwingine.

Ethan anajiuliza ikiwa atahisi safi au mwenye kustahili tena. Ameshindwa na kutumbukia kwenye vishawishi fulani mara nyingi sana kiasi kwamba anahisi kushindwa kujizuia na kujiuliza ikiwa amepoteza kabisa baraka zake alizoahidiwa. Anashangaa kama anaweza kusamehewa na anazidi kuhisi mwenye hatia kanisani.

Madison anapambana na ugonjwa wa lishe. Olivia ana ulemavu wa kujifunza. Conner anapambana na aibu ya imani (hatia ya kupita kiasi ya utovu wa maadili). Abigail amenyanyaswa na anahisi kama hana thamani. Wazazi wa Jake wanapitia talaka, naye anahisi kuumia na kuchanganyikiwa. Jayden alisalitiwa na hahisi kama anaweza kusamehe.

Watu wana mapambano mengi, lakini kuna suluhisho moja. Suluhu hilo lina jina—Yesu Kristo. Watu hawa wote wanataka kuhisi kuwa na nguvu, wasafi, wenye furaha na wazima tena, hata hivyo hawawezi kutatua matatizo yao wenyewe. Lakini Yesu Kristo anatoa msaada. Kwa kweli, kushughulikia udhaifu ndio utaalamu Wake. Usaidizi wake kwa kawaida hauji jinsi au wakati tunataka, lakini huja.

Hapa kuna baadhi ya kanuni za kutusaidia kukubali mwaliko wa Mwokozi wa kutembea pamoja Naye (ona Musa 6:34), hasa wakati wa kupambana na udhaifu.

Maisha Yanatakiwa Kuwa ni Mtihani

Mungu anakupenda wewe zaidi ya anavyopenda hali yako ya faraja na urahisi. Je, ni mashujaa wako wangapi wanaopata faraja na mafanikio pekee? Uwezekano mkubwa zaidi, wanakabiliwa na upinzani mkali na magumu mara kwa mara. Kama sehemu ya mtihani wetu katika maisha, Bwana anaonelea vyema kuwarekebisha watu wake; ndiyo, anajaribu subira na imani zao” (Mosia 23:21). Huenda tusipende, lakini mara nyingi majaribio yetu magumu zaidi hutupatia fursa za ukuaji usio na kifani.

Udhaifu Sio Ishara ya Kutokukubaliwa na Mungu

Watu wengi wa kale waliamini kwamba magonjwa ya kimwili au ya akili yalikuwa ishara ya adhabu ya Mungu (ona Yohana 9:2). Lakini udhaifu ni sehemu ya maisha inayoletwa na Anguko. Ingawa kupambana na changamoto ni sehemu ya kawaida na muhimu ya mpango wa Baba wa Mbinguni, kukabili mapambano hayo peke yake siyo mpango mzima. Yesu Kristo hakutumwa kutuhukumu; Alitumwa kuwapenda na kuwasaidia kuwarudisha wale waliopotea, dhaifu au wapweke—ambao ni sisi sote (ona Yohana 3:16–17; Luka 15).

Mambo Madhaifu Yanaimarishwa Kupitia Kristo

Ni muhimu kwamba tujifafanue wenyewe kwa muunganiko wetu wa agano na Kristo na kutegemea kwetu ukamilifu Wake badala ya kufafanuliwa na kutokamilika kwetu. Yesu Kristo hakuwaacha kamwe wanyonge waliomtafuta kwa bidii katika imani. Mungu huwapa watu “udhaifu ili wawe wanyenyekevu; na neema [Yake] inatosha kwa watu wote wanaojinyenyekeza mbele [Zake] … na kuwa na imani katika [Yeye],” na wakifanya hivyo, “basi [Atafanya] vitu dhaifu kuwa na nguvu kwao” (Etheri 12:27). Tunapoleta mahangaiko yetu kwa Bwana kwa moyo uliovunjika na roho iliyopondeka (ona 3 Nefi 9:20), Anaweza asiyaondoe mara moja, lakini Atatusaidia na kututia nguvu.

Kuwa na Subira na Wewe Mwenyewe

Njia ya agano ni safari ndefu sana, sio mbio fupi. Kufuata njia hiyo hutusaidia kupitia misukosuko na majanga mengi, heka heka, misisimko na hatari, mazuri na dhoruba za maisha. Unajifunza masomo mengi katika kila hatua kwenye safari hiyo. Neema ya Yesu Kristo mara nyingi hufunuliwa kila wakati, sio tu katika nyakati za kujitenga au matukio ya miujiza.

Picha
mvulana akionekana mwenye nguvu

Ungana na Kristo

Ikiwa unahisi u dhaifu au unatatizika, kubali mwaliko wa Mwokozi: “Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha” (Mathayo 11:28). Tafuta njia zinazokusaidia kuungana Naye. Unapomfikia, utagundua kuwa amekuwa akikufikia na hatakuacha kamwe! Maisha hayatakuwa kamili, wala hayatakuwa bila udhaifu, maumivu na mapambano. Lakini itakuwa bora ukiwa na Mganga Mkuu kando yako kukuinua unapoanguka, kufunga majeraha yako na kukuongoza katika njia zinazoongoza kwenye furaha ya kudumu.

Yesu Kristo ni mtaalamu wa kushughulikia udhaifu. Yeye ni mtaalamu wa kufanya kazi pamoja na wewe!

Chapisha