Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Fanikiwa Ukiwa na Mwokozi
Machi 2024


“Fanikiwa Ukiwa na Mwokozi,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Feb. 2024.

Nguvu ya Kujiandaa na Kuwa

Fanikiwa Ukiwa na Mwokozi

Mwokozi anakusaidia kutimiza matamanio yako ya haki kwa maisha yako ya baadaye.

Picha
Yesu Kristo akimkumbatia msichana

“Jitayarishe kwa ajili ya kesho yako.” Inaonekana huo ndio ujumbe nyuma ya mambo mengi katika maisha ya kijana—shuleni, kanisani, kazini, nyumbani. Unaweza kuanza kufikiri, “Ndiyo, ndiyo. Naelewa.” Bila shaka unajua kwamba siku zijazo zinakuja na unapaswa kujiandaa kwa hilo. Na kwa dhati kabisa, unataka kufanya maisha yako ya baadaye kuwa mazuri.

Unagundua kile kilichopo moyoni mwako mwenyewe. Unajifunza kile hasa unachokitaka. Unataka kufanya mambo mazuri na ya maana kwa maisha yako—kuweka alama yako katika ulimwengu na katika maisha ya watu wengine, kumtumikia Mungu na wanadamu wenzako. Unakuja kujua kwamba hii ni sawa na itakufanya uwe na furaha ya kweli.

Kwa hivyo, hapa kuna mambo mengine muhimu ya kujua unapokua na kujiandaa kwa siku zijazo:

  • Bwana anaujua moyo wako pia (ona Mafundisho na Maagano 6:16). Kwa sababu matamanio yako ya kina na ya dhati kwa ajili ya maisha yako ni mazuri na ya haki, Yesu Kristo yuko pamoja nawe ili kukuimarisha unapojiandaa.

  • Hujitayarishi tu kufanya mambo, wewe unakuwa yule Baba wa Mbinguni na Mwokozi wanajua unaweza kuwa.

  • Unaweza kufurahia sasa huku pia ukijiandaa kwa ajili ya siku zijazo. Wakati huu katika maisha yako ni wa kipekee, na maamuzi mazuri unayofanya yanakutayarisha kwa maisha mazuri ya baadaye.

Unapofikiria kuhusu kile unachojitayarisha, fikiria pia jinsi Mwokozi anavyokuimarisha njiani. Na fikiria kile anachokusaidia kuwa.

Unajiandaa Kwa Ajili ya Nini?

Hii ni baadhi ya mifano michache.

  • Elimu zaidi

  • Maagano ya hekalu

  • Misheni

  • Ndoa

  • Kazi na ajira

  • Familia na uzazi

  • Ufuasi wa maisha yote

Je, Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo Wanakuimarisha Vipi Pale Unapojiandaa?

Hii ni baadhi ya mifano michache.

  1. Wanakutumia Roho Mtakatifu, ambaye anaweza:

    1. Kukufariji.

    2. Kukuongoza.

    3. Kukutia moyo.

    4. Kukukumbusha mambo uliyojifunza.

    5. Kukupa ujasiri.

    6. Kukupa amani.

    7. Kutuliza woga wako.

  2. Wanawatia moyo manabii kukufundisha kupitia:

    1. Mkutano mkuu.

    2. Majarida ya Kanisa.

    3. Matangazo Maalumu.

    4. Tovuti za Kanisa na mitandao ya kijamii.

    5. Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi.

  3. Wanawahimiza wengine kukusaidia na kukuinua, ikiwa ni pamoja na:

    1. Wazazi.

    2. Marafiki.

    3. Viongozi.

    4. Walimu.

Yesu Kristo Anakusaidia Kuwa Nani?

Yesu Kristo anakusaidia kuwa zaidi kama jinsi Yeye alivyo—zaidi kama Baba yako wa Mbinguni.

Wanafurahi katika kila hatua ndogo unayochukua—kila andiko unalosoma, kila kazi ya Kanisa unayotimiza, kila kazi ya shule unayofanya kwa bidii, kila mtihani unaousomea, kila mazoezi unayohudhuria, kila neno la fadhili unalotamka, kila tendo la huduma unalofanya na mengi zaidi.

Kwa nguvu za Mwokozi, utakuwa umejitayarisha vyema kwa ajili ya maisha yako ya baadaye kuliko vile ambavyo ungeweza kuwa bila Yeye. Na utakuwa kitu kikubwa zaidi.

Chapisha